Timu ya anayochezea Muingeleza David Beckham, LA Galaxy imeifunga goli 3-0 timu anayochezea Mtanzania Nizar Khalfan, Vancouver Whitecaps, huku Nizar akiwa kwenye benchi katika mchezo wa MLS uliochezwa mapema hii leo.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Deport Center uliopo Carson,
California, LA Galaxy walikuwa wa mwanzo kutikisa nyavu kupitia kwa M. Magee katika dakika ya 40 na kwenda mapumziko LA Galaxy wakiwa mbele kwa goli hilo moja.
LA Galaxy walijipatia goli la pili katika dakika ya 64 kupitia kwa Robie Keane kabla ya M. Magee kukamilisha idadi ya magoli kwa kufunga goli lake la pili kwa siku ya leo na likiwa la tatu kwa timu yake.
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa LA Galaxy 3-0 Vancouver Whitecaps.
VIKOSI VILIVYOANZA.
LA GALAXY
12 J. Saunders
2 T. Dunivant
20 A. DeLaGarza
4 O. Gonzalez
23 D. Beckham
8 C. Birchall
30 P. Cardozo
10 L. Donovan
14 R. Keane
18 M. Magee
27 B. Jordan
VANCOUVER WHITECAPS
1 J. Cannon
4 A. Rochat
6 J. DeMerit
26 J. Harvey
25 J. Leathers
33 P. Vagenas
20 D. Chiumiento
28 G. Koffie
29 E. Hassli
22 S. Salinas
37 Camilo Sanvezzo
0 comments:
Post a Comment