TIMU ya soka ya Polisi Dar es Salaam imepata udhamini kutoka kampuni ya Home Shopping Center ya jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kuwa timu yake itashiriki michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, ambapo ikifanikiwa itacheza Ligi Kuu msimu ujao.
Alisema Polisi ilifanya vizuri katika fainali ya Ligi ya Taifa iliyofanyika Tanga mwezi uliopita na kuingia Ligi Daraja la Kwanza na sasa dhamira yao ni kufuzu Ligi Kuu.
Naye Said Gharib ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni hiyo alisema wameamua kutoa vifaa vya michezo ili viwasaidie katika maandalizi yao kwa ajili ya mashindano hayo. Alisema kwa kuanzia kampuni hiyo imetenga sh.milioni 60 na wametoa gari kwa ajili ya usafiri, viatu, jezi na mipira.
habarileo.co.tz
0 comments:
Post a Comment