vilabu

SIMBA, YANGA WATIMULIWA AZAM

Timu za Simba SC na Yanga SC zimetimuliwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mashabiki ambapo uwanja huo hauwezi kuhimili.

Ofisa habari wa Azam FC alisema kuwa wameuwandikia barua TFF kufuatia uwamuzi wa kusitisha mechi za Simba na Yanga kuchezwa katika uwanja huo uliopo Chamanzi na hivyo mechi za Simba na Yanga kupelekwa kwenye viwanja vingeni.

Simba na Yanga hapo awali walipanga kutumia uwanja wa Taifa kufuatia kufungiwa kwa uwanja wa Uhuru, lakini serikali wakauzuia uwanja wa Taifa na hivyo Simba kuamia Mkwakwani (Tanga) na Yanga kuhamia Jamhuri (Morogoro).

Baada ya TFF na vilabu husika kuomba kuutumia uwanja wa Taifa kwa mara ya pili walikubaliwa kwa masharti ya kucheza mechi mbili kwa wiki hivyo kupelea timu za Simba na Yanga kutafuta uwanja wake wa nyumbani kwa baadhi ya mechi ambazo hazitawezwa kuchezwa Taifa, na kutokana na sheria ya ligi ambayo hairuhusu timu kuwa na viwanja viwili katika mikoa miwili vya nyumbani na kukosekana uwanja mwingine jijini Dar es salaam ambao unaweza kuhimili mikiki ya ligi kuu, kulipelekea timu hizo kuhamishiwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi.

Kama Azam itaendelea na msimamo huo wakutotaka mechi za Simba na Yanga, basi moja kati ya haya yanaweza kutokea.
1. Kupanguliwa kwa ratiba mradi zipatikane mechi mbili kwa wiki ambapo Simba na Yanga wanakuwa nyumbani.
2. Simba na Yanga kuacha kuutumia uwanja wa taifa kutokana na kanuni ya ligi, na hivyo kurudi mkoani.
3. Kanuni ya ligi kupindishwa kuziruhusu simba na yanga kucheza mikoani na Taifa.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.