VPL

TEGETE AREJESHWA KUIVAA VILLA SQUAD

Uongozi wamabingwa wa Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati Yanga wamemrejesha kundini mshambuliaji Jerry Tegete.

Tegete aliondolewa kundini kwa utovu wa nidhamu na alisimamishwa kwa mda wa mwezi mmoja na kumpelekea akose michezo mitatu ya yanga ambapo yanga walishinda mmoja, kutoka sare mmoja na kufungwa mmoja, huku safu ya ushambuliaji iliyokuwa chini ya Mwape na Asamoah kuonekana kupoteza nafasi nyingi zaidi.

Yanga hii leo watakuwa kwenye uwanja wa Azam kuwakaribisha Villa squad katika muendelezo wa mechi za ligi kuu ya vodacom 'VPL'.

Villa squad wamesema hawatakubali kupoteza mchezo waleo baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo hivyo kujiweka katika mazingira magumu.

Yanga mchezo wao wa mwisho walipoteza kwa Azam FC na kupelekea viongozi kuanza kutadhimini uwezo wa kocha wao Sam Timbe, wanahitaji ushindi kuwapa matumaini mashabiki wao.


CCM KIRUMBA, Mwanza.

Baada ya Toto Africa kukubali kutoka sare na JKT Ruvu ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa kama ilivyo kwa Simba, hii leo watawakaribisha Simba SC katika uwanja ambao Simba wameapa kuto ufanya uwanja wake wa nyumbani chini ya meneja wa sasa.

Simba katika ziara zake zakanda ya ziwa huwa ni nadra kwake kutoka huko na point zote (lazima wapoteze point), na hivyo kupelekea mchezo huo kuwa mgumu kwake hii leo.


MKWAKWANI, Tanga.

Baada ya Azam FC kupata ushindi katika mechi zake mbili, leo watakuwa kibaruani cha kutaka kulipa kisasi kwa Coastal union ambayo imefanya vibaya katika mechi zake za hivi karibuni katika uwanja wa Mkwakwani.

Coastlal union waliwafunga Azam FC goli 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja huo wa Mkwakwani uliofanyiwa ukarabati na Azam FC.



Mchezo mwingine utakuwa mkoani Pwani katika uwanja wa Mlandizi ambapo RUVU SHOOTING watawakaribisha AFRICAN LYON.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.