Klabu za Simba, Yanga na Azam zipo mapumzikoni kupisha mechi za kusaka nafasi ya kushiriki kombe la mataifa ya Afrika mwakani katika nchi za Gabon na Equaterial Guinea.
Kupumzika kwa timu hizo haimaanishi kuu ligi kuu ya Vodacom imesimama, ila kuna michezo itaendelea wikiend hii na wikiend inayokuja kabla ya timu hizo kurejea katika ligi hapa Oktoba 15.
Wikiend hii kutakuwa na michezo mitano katika mikoa mitano tofauti.
JAMHURI, Dodoma.
Kesho katika uwanja wa Jamhuri Polisi Dodoma watawakaribisha majeruhi Toto Africa ya Mwanza. Toto walifungwa goli mbili na JKT Oljoro mchezo uliochezwa CCM Kirumba.
Katika msimu huu Polisi Dodoma wamekuwa wagumu kukubali kufungwa katika uwanja huo wajamuhuri, ambapo Toto Africa watataka kurudisha imani kwa mashabiki wake.
SHEIKH AMRI ABEID, Arusha.
Ni nafasi nyingine kwa Oljoro kuonyesha uimara wake katika ligi kuu ya vodacom pale watakapo wakaribisha Coastal union ya Tanga.
Coastal union ilipokea kipigo cha aibu toka kwa Yanga watakuwa na kazi ya kujinasua toka mkiani, huku ikiwa na changamoto ya kuondokewa na nyota wake watano wakutegemewa katika kikosi chake.
Oljoro toka wapoteze dhidi ya simba hawajapoteza mchezo wowote ule mpaka sasa ambapo wanashika nafasi ya tatu. JKT OLJORO Na COASTAL UNION zitapambana kesho oktoba mosi.
MANUNGU, Morogoro.
Baada ya kupokea kichapo toka kwa Simba Mtibwa Sugar watakuwa kibaruani pale watakapo wakaribisha Ruvu Shooting hapo kesho katika uwanja wa Manungu.
Ruvu Shooting ikiwa chini ya kocha wake Mkwasa watawakabili Mtibwa Sugar wakiwa na Kumbukumbu ya kumsimasha Azam FC katika uwanja wa Mabatini, ambapo Azam walilalama na refa kwa kushindwa kutafsiri sheria.
Mtibwa Sugar watakuwa kibaruwani bila ya Hussein Javu na Shaban Nditi walio itwa kwenye timu ya Taifa Taifa Stars. Watakuwa na kazi ya kusaka point tatu kuendelea kufukuzana na Azam FC pamoja na JKT Oljoro.
AZAM STADIUM, Dar es salaam.
Vijana toka Magomeni Mapipa, Villa Squad watakuwa kibaruani kujinasua toka kwenye mstari wa kushuka daraja pale watakapo wakaribisha vijana wa Tabata Moro united hapo kesho katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi.
Moro united ambayo inasafu kali ya ushambuliaji na safu dhaifu ya ulinzi watakuwa na kazi ya kutaka kujiweka pazuri katika msimamo.
Villa ambao walitoa sare na JKT Ruvu katika mchezo wake wa mwisho iko nafasi ya pili toka mwisho na kesho watakuwa na kazi ya kujinasua.
0 comments:
Post a Comment