VPL

Wakatamiwa wabanwa

Ligi kuu ya Tanzania bara imeendelea leo katika viwanja vinne tofauti, ambapo wakatamiwa wa Mtibwa Sugar na Kagera Sugar wameshindwa kutamba katika michezo yao ya leo.


JAMHURI, Dodoma.
Katika uwanja wa Jamhuri Mtibwa Sugar wameshindwa kumsogelea Simba baada ya kutoka sare ya 1-1 na Polisi Dodoma.

Mwenyeji Polisi Dodoma walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Juma Semsuye katika dakika ya 13 huku Mtibwa wakisawazisha goli hilo kupitia kwa Shabani Nditi katika dakika ya 70 ya mchezo.


AZAM STADIUM, Dar es salaam.

Katika uwanja wa Azam Moro United wamegawana point na JKT Ruvu baada ya kutoka sare ya 2-2.

Magoli ya Moro United yametiwa kimiani na Godfrey Wambura na Gaudence Mwaikimba wakati yale ya JKT Ruvu yakifungwa na Hussein Bunu na Alhaj Zege.


KAITABA, Kagera.

Kagera Sugar wamechapwa na Oljoro katika uwanja wake ambao ni ngumu kwa mgeni kutoka na ushindi na hivyo kuwa na hali mbaya. Kagera ambayo mpaka sasa haijashinda mchezo wowote mpaka sasa wamefungwa goli 2-1 na JKT Oljoro.

Magoli ya Oljoro yote mawili yalifungwa na Amir Omar, huku lile la kufutia machozi la Kagera Sugar likifungwa na Themi Felix.


MLANDIZI, Pwani.

Ruvu Shooting ya Pwani imeutumia vyema uwanja wake wanyumbani baada ya kuichapa goli 2-0 timu ya Africa lyon.

Magoli ya Ruvu yamefungwa na Kassim Linde na Abrahman Abdallah.


MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (7) 15
2. Azam FC (7) 14
3. Mtibwa Sugar (7) 12
4. JKT Ruvu (7) 11
5. Ruvu Shooting (7) 10
6. JKT Oljoro (7) 10
7. Toto Africa (7) 9
8. Yanga (7) 9
9. Moro United (7) 9
10. Africa lyon (7) 6
11. Polisi Dodoma (7) 7
12. Kagera Sugar (7) 5
13. Coastal Union (7) 4
14. Villa Squad
(7) 4

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.