VPL

Yanga wapeta Azam, Simba wavutwa

Uwanja wa Azam uliopo Chamanzi umeonekana kuwa na neema kwa mabingwa wa Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati Yanga kufuatia ushindi wa pili walioupata katika uwanja huo.

Yanga walikwaana na Villa squad katika uwanja wa Azam na mchezo kumalizika kwa Yanga kuchukuwa point zote tatu baada ya kuichapa goli 3-2.

Magoli yaliyowapa usingizi wanajangwani hii leo yalitiwa kimiani na Haruna Niyonzima, Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza wakati ya Villa squad yakifungwa na Mohamed Kijuso na Kiggi Luseke.

Akizungumza baada ya mchezo, msemaji wa Villa Squad alisema mwamuzi wa mchezo huo alishindwa kuumudu mchezo na kujikuta akiwabeba yanga na kuifanya timu yake kuchezea kichapo.


CCM KIRUMBA, Mwanza.
Kama ilivyo ada kwa Simba kuacha point katika kanda ya ziwa na safari hii wameacha point 4 kufuatia sare ya leo waliyo ipata huku mshambuliaji wa simba Felix Sunzu akiripotiwa kukimbizwa hospitalini baada ya kuumia.

Katika mchezo wa leo ulimshuhudia kipa Juma Kaseja akiingia nyavuni mara 3 na mchezo kwisha kwa sare ya 3-3, huku kukishuhudiwa mbwa wa polisi akiingia uwanjani na kuwafukuza Sunzu na Boban na hivyo mchezo kusimama kwa mda.

Magoli ya Simba yametiwa kimiani na Felix Sunzu aliyefunga mawili na Patrick Mafisango, wakati ya Toto yakifungwa na Dalington Enyima, Idd Mobi na Soud Mohamed.


MKWAKWANI, Tanga.
Ukisikia Azam FC kashinda msimu huu, basi moja ya goli limefungwa na John Bocco Adebayor ambaye kafunga magoli matano kati ya sita yaliyofungwa na Azam FC katika msimu huu.

Stori iliendelea kuwa ileile pale Bocco aliposhinda goli pekee la ushindi kwa Azam FC walipo karibishwa na Coastal union hii leo. Ilikuwa ni dakika ya 23 kipindi cha Kwanza kwa mkwaju wa penati Bocco alitia mpira kimiani na kufikisha magoli 5.

Coastal union walipata mkwaju wa penati katika kipindi cha pili ambapo waliipoteza na kupelekea mchezo kwisha kwa Azam FC kushinda goli moja bila.


MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (7) 15
2. Azam FC (7) 14
3. Mtibwa Sugar (6) 11
4. JKT Ruvu (6) 10
5. Toto Africa (7) 9
6. Yanga (7) 9
7. Moro United (5) 8
8. Ruvu Shooting (6) 7
9. JKT Oljoro (6) 7
10. Africa lyon (6) 6
11. Polisi Dodoma (6) 6
12. Kagera Sugar (6) 5
13. Coastal Union (7) 4
14. Villa Squad (7) 4

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.