kitaa

Nyota wa miaka 50 katika soka

Peruzi za kitaa kimetuwa kwenye mjadala wa kusaka mchezeji ambaye anaweza kuwa Icon katika miaka 50 ya uhuru.

Kitaa kimetua katika group la KANDANDA na kukutana na post ya Patrick Dumulinyi 'PD'

TWENDE KITAANI

Patrick Dumulinyi:
Katika Wachezaji waliowahi kuwika bongo..na kuitangaza Tasnia ya Kandanda kimataifa na kitaifa..Nani angweza kuwa kinara au galacha hata kuamua kuiweka sanamu yake nje ya Uwanja wa Taifa au makumbusho katika miaka hii 50?

Maoni jamani..najua wengine tuliwasikia kwa Redio Tanzania ila wengine tumewaona wakicheza kabisaa!

MAONI YA WADAU

Ismail Mohamed:
kwa ngazi ya vilabu inawezekana lkn national team hakuna kaka!

Ally Suru:
Sunday Manara aka Computer huyu nadhan anafaa kuwa Kinara..

Ismail Mohamed:
kwa kipi?tunaangalia mchango wa mtu kwa taifa au kwa sababu aliwekwa kwenye stemp?naamini pd unatafuta mtu kama milla wa cameroon, abeid pele wa ghana, opong weah wa liberia, na wengineo wengi waafrica!sisi tz mtu huyo hatuna!

Patrick Dumulinyi:
Yap ni kweli wa dizaini hiyo..lakini walau angeweza hata kuwekwa kwenye kitu ukaingia Makumbusho ukasema huyu alikuwa mwanaume kweli

Ismail Mohamed:
sijui sina profile kubwa kwa manara ila atleast naweza kumtaja lunyamila!

lunyamila nimemuona na naamini yeye wakati wake kwa afrika mashariki na kati alikuwa anarandana na marehemu moses chikwalakwala wa zambia ukanda huu kama miongoni mwa mawinga bora kupata kutokea!

Heri Issa:
Sunday Manara alikuwa ni mchezaji wa kwanza wa bongo kucheza mpira wa kulipwa nje. fuatilia history yake hapa

Charles Mulumbulila:
maulid dilunga, aliwahi kuwemo kwenye kombaini ya afrika

Heri Issa:
Charles Mulumbulila ni kweli dilunga na Mahadhi walikuwemo kwenye kombaini ya Afrika. Pia kwa wachezaji waliotoa mchango mkubwa wakuingia mashindano ya Afrika 80 atuwezi kumsahau Peter Tino kwani goli lake kule Zambia ndio liloipeleka Stars Lagos

Charles Mulumbulila:
Jela mtagwa mchango wake ni mkubwa

Heri Issa:
Tukihamua kutaja wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwa timu yetu ya Taifa ni wengi sana. Mtu kama Jela mpaka kwenye stamp za posta aliwekwa kwa kweli ulikuwa mkoba wa nguvu. Bado pia hatuwezi kumsahau pondamali ambaye alikuwa kivutio kikubwa hasa kutoka na mbwembwe zake kule Zambia na Lagos.

Patrick Dumulinyi:
Lakini we can get basi labda kwa kila muongo (Decade-Ten Years) nani alikuwa noma zaidi..theni hao wote tuwapambanishe nani aliukuwa noma zaidi. Pondamali barahh

Jerry Mwaikambo:
Mimi niliyeanza kufuatilia mpira miaka ya 90 nitamuweka Ally Mayai(Tembele) na Lunyamila...

Ismail Mohamed:
kwangu kwa miaka ya tisini kuna nemes, mwameja, zamoyoni malota na lunyamila! mmoja kati yao anaweza kuwa!

Frank Robert Rweyemamu:
80-90 aliyesahaulika ni Thuwein Ally Waziri....huyu alikuwa hatari, muulizeni hata Mbwiga atawaambia. Lagos wanamjua. Miaka ya 90-2000 braza Lunya alitisha....2000-2010 dah...hapa najiweka pembeni kuepuka ushahidi.....

Vicent Exavery:
Abdallah 'king' kibaden angalia historia yake kuanzia klabu hadi taifa akiwa mchezaji na kocha

Ismail Mohamed:
yah vicent now u can touch atleast the real modal whom i did forget!mputa naweza kusema kama mchezaji lakini pia ndiye kocha mwenye mafanikio kupita wooote tz kwa sasa aliipeleka simba fainali caf na si kama simba kuwa timu ya wahindi basi angeweza kuweka rekondi ya kipekee zaidi!king mputa anastahili kuwa pd!

Frank Robert Rweyemamu:
Sasa King kama mchezaji au Kocha???

Patrick Dumulinyi:
Itabidi huyu tumuache upande wa makocha kwanza

Israli Dunda:
For Mwameja na Marehem Ramadhani Lenny!

Heri Issa:
King Mputa hata kwa uchezaji alikuwa anatisha. Mimi napenda kutoa maono yangu kwa kuzingatia namba, nitaanza miaka ya 70 hadi 80, Golini ni mambosasa na Mahadhi, 2 Boi Idd wekencs 3, Kajole, Nne Tenga tano Jella, viungo ni Abdularahaman juma, Sunday manara, Haidari Abeid na halid Abeid, viungo, winga ni Willy Mwaijibe, Maulidi Dilunga na washambuliaji ni Kibadeni na Semburi, Miaka ya 80-90, General Mkambi, Masters Mkwasa, Mathematic Ahmed Amasha, Juma pondamali, Zamoyoni mogela, Mohamed Salim, Mukebezi, 90 kuja 2000, Lunyamila, masha, Issa athumani na mwameja. 2000 mpaka 2010 wana ruka ruka tu uwanjani hakuna mtu unaweza ukasema anatisha.

FUATILIA MJADALA

About kj

1 comments:

Anonymous said...

Mnamsahau Kenneth Mkapa, Kasongo,

Powered by Blogger.