CECAFA

Zanzibar waanza kwa kichapo


Timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' imeyaanza vibaya michuano ya Tusker Chalenje Cup hili leo baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Uganda.

Katika Mchezo huo ulioanza saa kumi alasiri katika uwanja wa Taifa ulishuhudia Uganda wakimiliki mpira kwa kiasi kikubwa, huku Wazanzibar wakiwa nyuma na kupoteza mipira kirahisi.

Kipindi Cha Kwanza kilikuwa kizuri kwa Uganda ambao walimaliza kipindi hicho wakiwa mbele kwa goli moja lililo fungwa katika dakika ya 40 Ochan akipokea pasi murua ya Emanuel Okwi. Huku wakipoteza nafasi kazaa ambayo ingewatoa mapumziko wakiwa na magoli ya kutosha.

Baada ya kipindi cha kwanza kuwa nyuma na kupoteza mipira ovyo, Kipindi Cha pili Zanzibar walicharuka na kucheza kwa kuonana katika dakika 15 za kwanza kabla ya kupotea na mpira kuwa wa butua butua.

Katika dakika ya 47 Zanzibar walisawazisha goli kupitia kwa Ally Badri Ally aliyeisumbua kwa kiasi fulani ngome ya Uganda. Katika dakika ya 74 Emanuel Okwi alimgusia Mark Serugama ambaye hakufanya ajizi zaidi ya kutumbukiza mpira kimiani, na kupelekea mchezo kurejea kwenye mikono ya Waganda, ambao waliibuka kidedea kwa goli 2-1.


Katika mchezo wa Awali Burundi iliipa kichapo cha kutosha Somalia cha magoli 4-1. Hivyo Burundi kuongoza kundi hilo ikifuatiwa na Uganda, Zanzibar, wakati Somalia wakibuluza mkia.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.