zanzibar

Mwaikimba aipa point Azam, Yanga washinda Mapinduzi


Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba ameipatia point moja timu ya Azam FC pale walipo wakabili Mafunzo FC walio wafunza Soka Yanga, huku Yanga wakiwachapa goli 2 bila Kikwajuni.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja Amani jioni ya leo, Mafunzo FC walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 12 kabla ya Mwaikimba kuisawazishia Azam FC.

Katika mchezo huo ulishuhudia urejeo wa Mrisho Khalfan Ngassa katika kikosi kufuatia jeraha alilolipata pale Azam FC walipocheza na Yanga mwaka jana katika mchezo wa kirafiki.

Katika mchezo wa pili ulichezwa saa mbili usiku katika uwanja wa Amani ulishuhudia Yanga ikizinduka na kukusanya point 3 kufuatia ushindi wa goli 2 bila walioupata kwa Kikwajuni leo.

Kutokana na matokeo ya leo Azam FC inabaki kileleni mwa Kundi B kwa kuwa na point 4, Mafunzo ikishika nafasi ya pili wakiwa na point sawa na Azam, wakati Yanga wakiwa na point 3 katika nafasi ya tatu.

Michezo ya mwisho kwa kundi B itachezwa ijumaa kwa kushuhudia Yanga ikisaka ushindi mbele ya Azam ili watinge nusu, huku Kikwajuni walio aga mashindano wakiwakabili ndugu zao Mafunzo.


Kesho kunamichezo ya kundi A,

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.