netball

8 zathibitisha kushiriki mashindano ya Mei Mosi

Evance Ng’ingo

TIMU nane zimethibitisha kushiriki michuano ya Mei Mosi itakayoanza Aprili 16 mpaka 29 mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi kitaifa, Award Safari ilizitaja timu hizo kuwa ni Idara ya Polisi Makao Makuu, Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC) Arusha, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mapinduzi Dodoma.

Timu nyingine ni Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA Dodoma), Wizara ya Mambo ya Ndani na Tumbaku (TTPL) ya Morogoro.

Safari alisema kuwa tarehe ya mwisho ya kuthibitisha ushiriki ni Machi 30 mwaka huu ambapo ni siku ambayo kutakuwa na mkutano wa viongozi wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi.

Alisema kuwa karibia timu 57 kutoka maeneo ya kazi ambazo zinaangukia kwenye Mashirikisho ya Michezo ya Shimmuta, Shimiwi, Shimisemita na Bammata zimealikwa kushiriki kwenye michezo ya Mei Mosi mwaka huu.

Alisema kuwa katika michuano hiyo ya mwaka huu inashirikisha michezo ya kuvuta kamba, kukimbia, Mbio za Baiskeli, Karata, Bao, Netiboli, Mbio ndefu na Drafti.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.