vilabu

CHINI YA KAPETI: JULIO KUTUA POLISI MOROGORO



Kocha msaidizi wa coastal union Jamhuri Kihwelo Julio yuko katika hatua za mwisho za kujiunga na Polisi Morogoro iliyositisha mkataba na kocha wao Adolph Richard wiki jana.

Julio ambaye aliipandisha ligi kuu timu ya Mwadui FC na kwenda kuwa kocha msaaidizi wa coastal union, anataraji kumwaga wino katika timu ya Polisi morogoro, inayo pambana kubaki ligi kuu ya vodacom.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia Julio alitaraji kumwaga wino wa kuifundisha Polisi usiku huu, kama maongezi yao ya mwisho yamekwenda salama na kujiunga na kikosi hicho haraka iwezekanavyo kwa ajili ya mchezo wa mwishoni mwajuma hili.

Julio anataraji kusaidiwa na Amri Saidi ambaye ndiye yuko na timu kwa hivi sasa, na jioni ya leo aliyongoza polisi morogoro katika maandalizi yake ya mchezo unao fuata wa ligi kuu ya vodacom.

Endapo dili la Julio kuifundisha Polisi Morogro, huenda akaweka rikodi katika soka la bongo kwa kufundisha timu tatu tofauti katika msimu mmoja, ambapo alianza na Mwadui FC, kisha Coastal union baada ya Mwadui kupanda ligi kuu na sasa huenda akahamia Polisi Morogoro.

Julio amekaa kwenye benchi la coastal union msimu huu katika michezo miwili ya ligi kuu ya vodacom ambapo coastal union ilishinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mwingine

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.