netball

Bandari kuinoa Taifa Queens

John Gagarini, Kibaha

TIMU ya mpira wa Pete ya Bandari ya Jijini Dar es Salaam inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Taifa Queens Mei Mosi mwaka huu.

Akizungumza mjini Kibaha mwenyekiti wa timu hiyo Athuman Mkangara alisema kuwa mchezo huo ni moja ya michezo ya majaribio watakayoifanya Taifa Queens kwenye maandalizi yake ya Kombe la Mataifa ya Afrika la Netiboli.

Mkangara alisema kuwa lengo la mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa na ligi daraja la kwanza itakayochezwa mkoani Mbeya Agosti mwaka huu.

"Tunaendelea na mazoezi makali kwa sasa timu iko kambini chini ya mwalimu Rose Walele na mchezaji mkongwe wa Bandari, Matalena Mhagama ili kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri kwenye ligi hiyo," alisema Mkangara.

Alisema kuwa timu yake inatarajia kucheza na timu ya Filbert Bayi ili kujipima nguvu kujua udhaifu uko sehemu gani ili waweze kuboresha timu kwa ajili ya kuleta mafanikio.

"Hadi sasa timu imeonyesha uwezo mkubwa kwani mara baada ya kupanda daraja imecheza michezo mitatu ya majaribio na kushinda yote," alisema Mkangara.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.