CAF

Simba kukwaana na Wasudani katika Raundi ya 3


Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho CAF, Simba SC sasa watawavaa El Ahly Shandy ya Sudan baada ya El Ahly Shandy kuwachapa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji jumla ya magoli 3-0.

Katika mchezo wa leo El Ahly Shandy wameibuka na ushindi wa goli 2-0 kwenye Mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa huko Mjini Shandi, Mji ambao uko Kilomita 150 Kaskazini Mashariki ya Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum.

Bao zote 2 za El Ahly Shandy zilifungwa na Nadir Eltayed katika Dakika za 14 na 60. Hivyo El Ahly Shandy wamewatoa Ferroviario de Maputo kwa jumla ya bao 3-0 baada ya pia kuwatungua huko kwao Maputo bao 1-0.

Simba waliwabwaga ES Setif kwa bao la ugenini baada ya kuwanyuka 2-0 Jijini Dar es Salaam na wao kuchapwa 3-1 huko Setif, Algeria.

Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kati ya Simba na El Ahly Shandy itachezwa Dar es Salaam Uwanja wa Taifa hapo Aprili 29 na marudiano huko Shandi, Sudan kati ya Mei 11, 12 na 13.

About kj

3 comments:

Anonymous said...

Nashukuru sana kaka. Hii habari nimeitafuta mpaka kwenye site ya CAF nimeikosa. Nimefurahi sana kuipata hapa, thanks a lot...

Anonymous said...

Shukran Mwandishi!
www.sokainbongo.com

Anonymous said...

ngoma nzito nyingine kwa simba,, si mbaya tupo pamoja nao

Powered by Blogger.