JEMBE LA MAXIMO LA SHINDWA KUCHOMOZA KWA MWAPE NA ASAMOAH
Ukitaja orodha ya wachezaji waliyo ibuliwa na kocha mkuu wa timu ya taifa katika miaka ya 2006-2010, Marcio Maximo hukosi jina la mshambuliaji aliyeshindwa kufurukuta na kuchomoza mbele ya Davis Mwape na Kenneth Asamoah msimu uliokwisha. Na huyo si mwingine ni Jerry Tegete.
Jerry Tegete alikwisha tabiriwa kushindwa kutamba katika ligi kuu ya Vodacom msimu huu, kufuatiwa na urejeo wa Kenneth Asamoah ambapo aliunganisha nguvu na Davis Mwape aliyecheza nusu msimu katika msimu wa 2010/11.
Baada ya msimu wa 2010/11 kwisha na uvumi wa urejeo wa Keneth Asamoah kusikika, Tegete alianza kusaulika lakini alirejea kwenye michuano ya Taifa Cup ambapo alimaliza michuano hiyo na magoli 6 akiwa nyuma kwa goli 2 toka kwa kinara Gaudence Mwaikimba.
Alicheza vyema katika michuano hiyo na kujenga taswira ya yanga yenye safu kali ya ushambuliaji lakini mambo yakawa kinyume, kwa kuwa na safu mbovu ya ushambuliaji iliyo kuwa ina wategemea wageni watatu Asamoah, Mwape na Hamisi Kiiza.
Tegete makali yake ya Taifa Cup yalipotea na kuanza kukaa benchi na pale alipopata nafasi alishindwa kufanyia kazi na mwisho wa siku kumaliza msimu wa ligi kuu ya Vodacom bila ya kuziona nyavu.
Kwa sasa Tegete anavumishwa kwenda Simba, je akifanikiwa kwenda Simba ama akibaki Yanga atafanikisha kurejesha ustadi wake wa kufumania nyavu.
0 comments:
Post a Comment