mtazamo

NATAMANI KUWAONA WAKICHEZA PAMOJA

Ligi kuu ya vodacom imemaliza jumapili iliyopita kwa Simba SC kutwa ubingwa, huku ikiniachia nyota 11 ambao naota kuwashuhudia wakicheza pamoja na nyota hao ni:

KIPA

JUMA KASEJA

Juma Kaseja amekuwa akinivutia toka mwanzoni mwa miaka 2000, amekuwa bora mlingotini na kupelekea mashabiki kumuita Tanzania One.

Kaseja kacheza michezo yote ya ligi kuu ya vodacom msimu huu, na ni ngumu kumuweka benchi akiwa mgumu kiafya.


BEKI

ERASTO NYONI

Beki huyu anaemudu kucheza nafasi zote za nyuma msimu uliokwisha alimudu vyema katika nafasi ya kulia ya Azam FC na kupelekea Ibrahim Shikanda kungojea kwenye benchi.

Nyoni kacheza michezo yote muhimu ya Azam FC na amekuwa na msaada mkubwa katika kuhakikisha Azam FC haifungwi magoli ya kizembe.

JUMA ABDUL

Dogo aliyemfanyia kazi nzuri Jamhuri Kihwelo Julio katika safari ya kusaka nafasi ya kushiriki Olympic, msaada huo umeonekana katika timu yake ya Mtibwa akicheza pande zote mbili za beki, akitoa pasi za goli pamoja na kuwa na bahati na mipira ya adhabu ndogo.

KELVIN YONDAN

Yondani amekuwa msaada mkubwa kwa simba sc toka viongozi wa timu hiyo wamrejeshe kundini. Simba imekuwa imara katika nafasi ya ulinzi kutokana na uimara wa beki huyu wakati.

AGGREY MORISE

Ukitaja mabeki bora wakati nchini kwa hivi sasa uwezi kuliacha jina la nahodha wa Azam FC Agrey. Chini yake akisaidiana na Moradi walitengeneza ukuta mgumu ambao haujawahi kutengenezwa na kikosi cha Azam FC toka ingie ligi kuu.


VIUNGO

PATRICK MUTESA MAFISANGO

Kati ya wachezaji walioifanya Simba kuwatishio msimu huu ni kiungo Mafisango aliyetolewa swadaka na Azam FC kwenda kwa simba.

Amekuwa akiisaidia Simba SC katika ulinzi na vilevile katika kuipeleka mbele mashambulizi na kufunga magoli muhimu.

Amekuwa akifika kwa wakati eneo analo hitajika na pale simba ilipo kuwa inamkosa ilionekana kutetereka.

HARUNA NIYONZIMA

Pamoja na Yanga kufanya vibaya msimu huu lakini katika eneo la kati la uwanja lilikuwa linaonyesha uhai kutokana na uwepo wa huyu Mnyarwanda aliyesajiliwa na Yanga akitokea APR.

Niyonzima na Hamisi Kiiza ndio wachezaji wangu bora toka kwa yanga msimu huu.


MWINYI KAZIMOTO

Kazimoto ameendeleza kuudhihirishia umma wa kitanzania kuwa ni bora katika eneo la kati ya uwanja. Amekuwa akiunganisha vyema Simba SC toka siku ya kwanza kuvaa uzi mwekundu katika uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga katika Fainali ya Kagame ambapo alicheza kwa dakika 17 za mwanzo.


WASHAMBULIAJI

HARUNA MOSHI BOBAN

Sifa yake ni moja anajuaa nini cha kuufanyia mpira, pasi zake, na namna anavyojipanga uwanja na namna anavyo funga magoli yake kwa ustadi unamfanya endelea kuwa bora kwa kizazi hiki cha soka cha Tanzania.

JOHN RAPHAEL BOCCO

Mshambuliaji huyu toka Azam FC huu ni msimu wake watatu mfululizo anafunga magoli zaidi ya 12 kila msimu na safari hii amefanikiwa kuibuka mfungaji bora baada ya kufikisha magoli 19.

EMMANUEL OKWI

Balaa la Mganda huyu anae kipiga Simba SC muulize mkongwe Nsajigwa, mabeki wa ES Setif, na El Ahly Shandy.

Mashambulizi ya Simba yamekuwa yakipitia kwa huyu Mganda na amefanikisha kumaliza msimu akiwa na magoli 13.


WA AKIBA

Mwadini Ally (Azam FC)
Shomari Kapombe (Simba SC)
Said Swedi (Coastal Union)
Salum Abubakari (Azam FC)
Hamisi Kiiza (Yanga SC)
Nsa Job (Villa Squad)
Nadir Ally Haroub (Yanga)

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.