CAF

SIMBA SAFARI YA HITIMISHWA JIJINI SHANDY, OKWI AFICHWA


Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC imetolewa katika michuano ya kombe la shirikisho Africa kwa mikwaju ya penalti 9-8 mbele ya El Ahly Shandy katika jiji la Shandy, baada ya kuruhusu nyavu zao kuguswa mara 3.

Katika mchezo wa leo uliomalizika hivi punde, ambapo Emanuel Okwi alishindwa kuonyesha cheche zake, Simba SC walianza vyema kwa kumudu mashambulizi ya Shandy nao kupeleka mashambulizi kadhaa katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Katika dakika ya 31 nusura Simba SC wapate goli la kuongoza baada ya Uhuru Suleiman kushindwa kutumia nafasi aliyopewa, ambapo kipa wa Shandy aliyekuwa katika kiwango chake kupangu shuti la Uhuru na mpira kugonga mwamba wa juu na kuzalisha kona ambayo nusura Mafisango aiandikie goli Simba lakini kipa huyo alikuwa kizingiti kwa simba.

Kipindi cha kwanza kuta ya Simba ilifanya kila jitihada kuokoa hatari zote na kupelekea timu hizo kwenda mapumziko bila kushuhudia nyavu kutingishwa, huku mchezo ukionekana kubalance kwa kushambuliana kwa zamu.

Kipindi Cha pili kilikuwa kibaya kwa Simba SC kwa kuruhusu goli katika dakika ya 46 lililo fungwa na Farid Mohammed na dakika 3 mbele Shandy waliandika goli la pili, na Shandy kuanza kulisakama goli la Simba SC.

Dakika ya 59 kujiamini kwa Victor Costa kulipelekea kwa Shandy kunasa mpira uliotumwa kwa Farid Mohammed na bila agizi akaifungia Shandy goli la 3 na kupelekea dakika 90 kumalizika kwa El Ahly Shandy 3-0 Simba SC na kupelekea matokeo ya jumla kusomeka 3-3 kutokana na goli 3 walizopata jijini Dar es salaam.

Changamoto ya mikwaju ya penati ikachukua nafasi na Simba wakapoteza penati 2 kati ya 10 walizo piga hii leo. Waliokosa penati kwa upande wa Simba ni Patrick Mutesa Mafisango penati ya pili na Juma Kaseja penati ya 10, ambapo kipa wa Shandy alizicheza penati hizo mbili wakati kwa Juma Kaseja akicheza penati moja.

Waliopata penati za Simba ni Victor Costa, Kelvin Yondan, Amir Maftah, Salum Machaku, Shomari Kapombe, Emanuel Okwi, Felixs Sunzu na Mwinyi Kazimoto.

Kikosi cha Simba kilichotolewa katika mashindano hii leo: Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Victor Costa, Kelvin Yondan, Mwinyi Kazimoto, Uhuru Suleiman/Salum Machaku, Patrick Mafisango, Felixs Sunzu, Haruna Moshi na Emanuel Okwi

About kj

2 comments:

Anonymous said...

Rudini home Wekundu tule Pilau maana mpira hatuwezi. Mpira ni fitina sisi tunaleta sanaa.

solomoni said...

Tunawasubiri tuje tuendeleze mpira wa udaku bongo...mlisema sana, asante ShAnDy kwa kuwazaba hao vidomodomo.....!!!!!!!!...

Powered by Blogger.