judo

Chief Kiumbe afanya kweli judo Tanzania

Na Elizabeth John

BAADA ya kuteseka kwa kukosa maskani maalumu tangu kuanzishwa kwake, hatimaye Chama cha Judo Tanzania (JATA), kimepata ofisi ya kudumu ambapo tayari wameanza kuifanyia kazi.

Rais wa chama hicho, Khalifa Kiumbemoto, ‘Chief Kiumbe’ aliiambia Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana kuwa ofisi hiyo waliyoanza kuitumia hivi karibuni, imegharimu sh milioni 32 hadi kukamilika kwake.

“Chama chetu bado ni kichanga, hivyo hakina fedha hata kidogo, gharama za ofisi hizo nimejitolea mfukoni mwangu kutokana na mapenzi yangu binafsi, baada ya kuona hatuna pa kufanyia kazi,” alisema Kiumbemoto.

Alisema kwamba mchezo wa judo ulikuwa hauna mlezi tangu kuanzishwa kwake, lakini kwa sasa wamepata mlezi wa kudumu ambapo atajitahidi kukihudumia kwa nguvu zote chama hicho.

Aliongeza kuwa kwa sasa chama hicho kina tovuti mpya inayojulikana na viongozi wote wa chama hicho, tofauti na ile ya awali ambayo ilikuwa inajulikana na mtu mmoja ambaye ni Katibu Mkuu wao, Kashinde Bundala.

“Mbali na gharama za ofisi, kubadilisha mtandao unaojulikana kwa jina la ‘Judo Tanzania’ kumenigharimu dola 2,500 za Marekani, ambapo nina imani Mungu atatusaidia tutapiga hatua na kupata mafanikio, inachohitajika ni moyo wa kujituma kwa viongozi wenzangu,” alisema.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.