Mdudu Muungano katika michezo
Katika miaka ya hivi karibuni tulipata kusikia mvurugano kati ya CHANETA (Chama Cha Netball Tanzania) na CHANEZA (Chama cha netball Zanzibar) na mara kwa mara tumekuwa tukisikia malumbano kati ya TFE (Shirikisho la soka Tanzania) na ZFA (Chama cha Soka Zanzibar).
Muda mwingi umetumika kuondoa mitifuano hiyo na mda mwingine kupelekea michezo husika kudorora kwa vipindi hivyo vya mitifuano, ambapo kwa kiasi kikubwa umesababishwa kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kushindwa kushughulikia mapungufu ya muungano.
Mdudu huyo wa muungano ambaye kwa sasa ametulia, anaweza kuibuka kama mjadala ulioibuliwa na moja ya redio nchini kutakwa timu za taifa kubadilishwa majina yao na kupewa moja ya vitu vinavyo itambulisha Tanzania, ambapo kwa kiasi kikubwa havi usishwi na muungano.
Kwa kuwa timu hizo zenye majina ya Taifa Quens (timu ya taifa ya Netball) na Taifa Stars (timu ya Taifa ya Soka) ni za upande wote mbili za Muungano na itakuwa ngumu kwa pande moja kukalia kimya kuona timu hizo zinatumia vivutio vya upande mmoja.
Kama mjadala huo utazalisha mchakato wa kusaka majina ya timu hizo za taifa lazima wawe makini katika uteuzi wa jina ambalo haliegemei upande wowote ule wa Muungano, lakini liwe linachochea uwepo na udumisho wa Muungano.
Kupitia michezo watu wameweza kuondoa tofauti zao na kuwa kitu kimoja. Kunahaja kubwa ya kubadilisha majina ya timu hizi mbili, lakini majina yatakayopewa lazima yawe yanadumisha umoja na muungano tulio nao.
0 comments:
Post a Comment