mtazamo

Je wajua haya ndani ya Kagame 2012

Yanga wamefanikiwa kutetea ubingwawake wa michuano ya kombe la Kagame linalo husisha vilabu bingwa toka katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kwa kuifunga Azam FC goli 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa hapo juzi katika uwanja wa Taifa jijini Dat es salaam.

Katika michuano hiyo kuna matukio kadhaa yamejiri kama ilivyo katika michuano mbalimbali inayofanyika ulimwenguni na haya ni baadhi ya matukio ambayo yamejiri na yaliyo karibia kuweka rikodi;


AZAM KUTWAA UBINGWA

Timu kadhaa zimeshawahi kushiriki kwa mara ya kwanza na kutinga fainali na kutoka patupu kama kilichotok Azam FC ambayo ilikuwa ni mara ya kwanza inashiriki michuano hiyo. Je wajua kama Azam wangechuluwa taji Aggrey Morisse angeingia kwanye vitabu vya kumbukumbu?

Katika mchezo wa soka ni nadra kushuhudia timu yenye jezi namba 13 uwanjani katika mchezo wa fainali kuibuka na ushindi, hususani katka mashindano makubwa. Msalaa huu wa jezi namba 13 umemkumba Michael Ballack na nyota wengine wengi.

Katika historia ya kombe la Dunia ni mchezaji mmoja aliyenyanyuwa kombe la dunia akiwa na jezi namba 13 ambaye ni raia wa Ujeruman Mullar. Hivyo basi kama Azam FC wangechukuwa kombe la Kagame basi nahodha wake Aggrey Morrise anae vaa jezi hiyo namba 13 angekuwa miongoni mwa wachezaji kutwaa taji kubwa akiwa ndani uzi namba 13.


NAZI YAVUNJWA TAIFA

Katuka mchezo wa robo fainali kati ya Azam na Simba nazi ilivunjwa katika uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam ikiashiria imani za kishirikina, ambapo vikosi vya timu hivyo havikutumia lango kuu kuingia uwanjani siku hiyo ya mchezo, ambapo ulikwisha kwa Azam kuichapa Simba goli 3-1.


TUSKER KUTOKA BILA NYAVU ZAO KUGUSWA

Mwakilishi wa Kenya mwaka huu Tusker ndio Timu pekee iliyo maliza mashindano hayo bila kufungwa goli lolote lile, baada ya kuondoshwa kwenye michuano hiyo wakiwa na point 2, baaada ya kutoka sare ya bila kufungana na Azam FC na Mafunzo FC waliokuwa katika kundi B.

Wakati Tusker wakimaliza bila kufunwa WAU Salaam toka Sudan Kusini ndio iliyofungwa goli nyingi mwaka huu baada ya kufungwa goli 17 huku wao wakifunga goli 1.


MWANACHAMA MPYA
 
CECAFA wamepata mwanachama mpya ambae ni Sudan Kusini na kwa mara ya kwanza wametoa timu kushiriki katika michuano ya chama hicho, ambapo waliwakilishwa na Wau Salaam, huku Somalia, Eritrea, Ethiopia na Sudan Kasakzini wakishindwa kutuma wawawkilishi wao mwaka huu.


PACHA HATARI

Kila kocha ulimwenguni wanaangaika kutengeneza mapacha katika safu ya ushambuliaji. ila kwa kocha mpya yanga Tom aikumpa kazi kubwa kupata washambuliaji mapacha, ambao kwa mara ya kwanza walikuwa wa nacheza pamoja katika michuano hiyo ambao ni Saidi Bahamuzi aliyesajiliwa na Yanga toka Mtiwa Sugar na Hamisi Kiiza kwa pamoja wakiwa wamefunga goli 12 kati ya magoli 14 yaliyofungwa na Yanga katika michuano hiyo.

Bahamuzi aliyeibuka kinara katika kufumania nyavu kwa kuingiza mpira nyavuni mara 6 sawa na Hamisi Kiiza na Taddy, Bahamuzi akiwapiku wapinzani wake kwa kigezo cha dakika chache alizo onekana uwanjani ukilinganisha na Kiiza na Taddy wa AS Vita.


 

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.