zanzibar

Simba na All stars, Azam na falcon nusu

Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC itaivaa Zanzibar All Stars katika mchezo wa nusu fainali la kombe la urafiki (ujirani mwema) lanaloendelea katika uwanja wa Aman uliopo Visiwani Zanzibar.

Hatua ya nusu fainali inataraji kufanyika siku ya jumatatu (julai 9) ambapo pia Azam FC watachuana na Super falcon wakati Simba wakikabiliana na All Stars.

Fainali itachezwa siku ya jumatano (julai 11) katika uwanja wa Aman Zanzibar, ambapo washindi wa michezo ya jumatatu julai 9 wataonyeshana ubabe katika kulisaka taji hilo lililoandaliwa kwa mara ya kwanza na chama cha soka Zanzibar 'ZFA'.

About kj

3 comments:

Anonymous said...

Hello Simba, sisi kama mashabiki wa timu yetu we're praying for you to ruin any upcoming team.Hongera kwa hatua mlofikia,hapo kesho do all the best.

Anonymous said...

Simba tupeni raha leo

Anonymous said...

Simba leteni ubingwa katika mtaa wa Msimbazi

Powered by Blogger.