Wikend

Wikend hii: Michuano ya Kagame kuanza

Michuano ya kombe la Kagame linalo shirikisha timu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, inataraji kulindima wikiend hii katika viwanja vya Chamanzi, na Taifa ambapo Simba, Yanga na Azam zitashuka dimbani. Wakati michuano ya Copa cocacola 2012 yakifikiwa Tamati.


KAGAME CUP

Mechi za Kagame Cup wikend hii ni:

Jumamosi (14/07/12)
APR Vs WAU SALAAM , Uwanja wa Taifa saa 8 mchana
YANGA Vs ATLETICO, Uwanja wa Taifa saa 10 alasiri

Jumapili (15/07/12)
AZAM FC Vs MAFUNZO, Uwanja wa Azam (Chamanzi) saa 10 alasiri
VITA CLUB Vs PORTS, Uwanja wa Taifa saa 8 mchana
SIMBA SC Vs URA, Uwanja wa Taifa saa 10 alasiri


NGORONGORO Vs RWANDA U20

Timu ya Taifa ya Rwanda ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 inatarajia kuwasili Dar es Salaam leo mchana (Julai 13 mwaka huu) kwa ndege ya RwandAir kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ngorongoro Heroes.

Rwanda yenye msafara wa watu 27 wakiwemo wachezaji 20 itafikia hoteli ya Sapphire. Mechi hizo zitachezwa Julai 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi na Julai 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa.

Ngorongoro Heroes tayari iko kambini chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Adolf Rishard kujiwinda kwa mechi hizo ambazo ni sehemu ya maandalizi ya kuivaa Nigeria.

Mechi dhidi ya Nigeria ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


FINAL COPA COCA COLA

Mwanza imejipatia tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Julai 13 mwaka huu) kuilaza Temeke mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. Mwanza walitangulia kufunga dakika ya tatu kupitia kwa Jamal Mtegeta kabla ya Temeke kusawazisha kwa penalti dakika ya 56 iliyowekwa wavuni na Baraka Ntalukundo.

Mabao mengine ya Mwanza yaliyoipatia tiketi ya kucheza fainali keshokutwa (Jumapili) yalifunga katika dakika 30 za nyongeza. Mtegeta alitikisa wazu dakika ya 94 kabla ya Dickson Ambundo kukwamisha la tatu dakika ya 108.

Nusu fainali ya pili itachezwa leo jioni ikikutanisha timu za Morogoro ambayo kwenye robo fainali iliibamiza Mara mabao 4-0 na Tanga iliyopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma
 

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.