mtazamo

JE OLJORO WATAENDELEA KUWAPA FURAHA WAKAZI WA ARUSHA?

KIKOSI CHA JKT OLJORO KILICHO SHIRIKI LIGI KUU 2011/12
JKT Oljoro iliwashangaza wadau wa soka namna ilivyo iwakilisha jiji la Arusha katika ligi kuu Tanzania Bara katika msimu wake wa kwanza, baada ya kumaliza duru la kwanza wakiwa nafasi ya 4, huku wakimaliza ligi wakiwa nafasi ya 6.

Katika msimu huu mpya utakao funguliwa agosti 25 kwa mchezo wa ngao ya jamii kati ya Simba na Azam, mashabiki wa soka toka jijini Arusha wanataraji makubwa toka katika kikosi hiki kinachomilikiwa na jeshi la kujenga Taifa.

Kama ilivyo ada kwa timu zinazofanya vyema kupoteza wachezaji wao nyota kwa kujiunga na Simba SC ama Yanga SC, Oljoro itakuwa bila ya mlinda mlango wake Hamad aliyejiunga na Simba kuziba nafasi ya Ali Mustapha 'Bathez' aliyejiunga na Yanga.

Wakiwa wameongeza baadhi ya wachezaji katika kikosi chao, swali linabakia kuwa, wataendelea kuwa Tumaini la Arusha, na kupunguza idadi ya michezo waliopoteza katika uwanja wake wa nyumbani toka kwa miwili mpaka kumaliza ligi bila kupoteza mchezo wowote ule katika dimba la Shekh Amri Abeid jijini Arusha.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.