vijana

Ngorongoro muendelezo wa vilio, waondolewa

Timu ya vijana ya Tanzania 'Ngorongoro Heroes' leo imekubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa Nigeria, na kuondolewa katika kinyanganyiro cha kuwania kushiriki Mataifa ya Afrika kwa soka la vijana wenye umri huo kwa jumla ya goli 4-1.

Ngorongoro Heroes walikubali kufungwa na Nigeria goli 2-1 katika mchezo wa awali uliopigwa katika uwanja wa Taifa kabla ya leo kupokea kichapo hicho cha goli 2-0.

Matokeo hayo ya leo ni muendelezo mmbaya wa kocha mpya wa vijana Jakob Michelsen, ambapo ameiongoza timu hiyo katika mchezo wake wa nne na kupoteza michezo yote, ikiwa ni michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Rwanda na miwili ya mashindano dhidi ya Nigeria.

About kj

2 comments:

Anonymous said...

Tunasafari ndefu kwenye michezo kama ilivyo kwenye maendeleo ya nchi.Bila kufumua mifumo yetu ya vyama vya mipira ni kilio kila mwaka

Anonymous said...

wanatia aibu hawa jamaa wanaondoka na maneno ya matumaini,oh tumerekebisha makosa kumbe ndo wanazidisha makosa. Bora wasingeenda huko.wanatia taifa hasara. Yaani hata hapa walifungwa. Kweli inaumiza vichwa.

Powered by Blogger.