Wikend

Wikend HIi: Ngorongoro kibaruani, Super 8 makundi kuhitimishwa

Habari za masiku wapenzi wa Sports In Bongo wikend, baada ya kuadimika kwa majuma matatu sasa tumerejea tena na mwisho wa juma hili kutakuwa na michezo kadhaa ndani ya Tanzania, wakati timu ya Taifa chini ya miaka 20 "Ngorongoro Heroes" wakiwa nchini Nigeria.


KUFUZU MATAIFA YA AFRIKA U20

Timu za vijana chini ya umri wa miaka 20 za mataifa mbalimbali Afrika zitakuwa katika kinyanganyiro cha kusaka tiketi ya kufuzu mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo, ambapo Tanzania (Ngorongoro Heroes) watakuwa wageni wa Nigeria, wikend hii.

Mchezo baina ya Ngorongoro na Nigeria unatarajiwa kuchezwa jumapili (agosti 12), ukiwa ni mchezo wa marejeano baada ya ule wa awali kufungwa goli  2-1 katika uwanja wa Taifa.

Hivyo basi kikosi hicho, ambacho kitashuka dimbani bila ya mfumania nyavu wa vikosi vya vijana Thomas Ulimwengu anaekipiga katika timu ya TP Mazembe ya nchini DR Congo, kitaitaji ushindi wa goli 2-0 katika mchezo huo.

Kwa iaka ya hivi karibuni timu za taifa za vijana za Tanzania zimekuwa na wakati mgumu pale wanapo kutana na Nigeria katika mashindano mbalimbali.


BANCK ABC SUPER 8

Hatua ya makundi ya michuano mpya ya BancABC Super 8 inayohusisha timu za Tanzania Bara na Visiwani ina hitimishwa jumapili kwa michezo minne katika viwanja vya mikoa minne katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.






Michezo ya mwisho kwa kundi A itawakutanisha SIMBA SC dhidi ya ZIMAMOTO katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, wakati JAMHURI ikiwakabili MTENDE RANGERS katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi jijini Dar es salaam.

Katika kundi B, SUPER FALCON watawakabili vinara wa kundi hilo MTIBWA SUGAR katika uwanja wa Amaan uliopo Zanzibar, wakati AZAM FC wakipepetana na POLISI MOROGORO katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.