Wikend

AZAM MDOMONI KWA MTIBWA, JKT NA YANGA

Ligi kuu ya Zanzibar na Tanzania Bara itaendendelea mwishoni mwa juma hili ambapo michezo inayotazamiwa na wadau wengi AZAM Vs MTIBWA, JKT RUVU Vs YANGA na SUPER FALCON Vs JAMHURI.


ZANZIBAR GRAND MALT PREMIER LEAGUE

Ligi kuu ya Zanzibar itaingia mzunguko wa 3 kwa michezo minne ambapo siku ya jumamosi SUPER FALCON itaikabili JAMHURI katika uwanja Gombani na katika Uwanja wa Amani kutakuwa na mchezo baina ya KMKM na BANDARI,

Siku ya jumapili (september 23) kutakuwa na michezo miwili ambapo MAFUNZO na MALINDI wakimenyana katika uwanja wa Amaan na Gombani kutakuwa na mtanange kati ya CHIPUKIZI na DUMA.


YANGA SC Vs JKT RUVU

Ni nafasi nyingine kwa Yanga kudhihirisha ubora wake baada ya kupoteza dhidi ya Mtibwa Sugar na kutoka suluhu dhidi ya Prisons, pale watakapo wakabili wazee wa kapeti JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa, hapo jumamosi.

JKT Ruvu wenye point 3 baada ya kufungwa na Simba na kuifunga Ruvu shooting, watakuwa na dhamira ya kuendeleza machungu kwa Yanga.

Yanga wamekuwa wakipata ushindi pale wanapokutana na JKT Ruvu, ila haitokuwa ajabu kama mambo yakiwaendea kombo hapo kesho.


AZAM FC Vs MTIBWA SUGAR

Baada ya Mtibwa Sugar kuigalagaza Azam FC katika michezo yote waliyokutana ndani ya msimu wa 2011/12, je Azam wataweza kuwarudisha vijana wa Mecky Mexime kwe mashamba ya miwa vichwa chini hapo jumamosi (sep 22)?

Mchezo huo utakao chezwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi unanogeshwa na namna Mtibwa Sugar walivyo uwanza msimu kwa kutoka suluhu na Polisi Moro kabla ya kuwazalilisha Yanga katika uwanja wa Jamuhuri.

Msimu huu Mtibwa Sugar wanaviungo wanao ichezesha timu vizuri na kuifanya iwe imara katika umilikaji wa mpira tofauti na misimu iliyopita, huku wakizidi kuimarika katika safu yao ya ulinzi.


MICHEZO MINGINE YA LIGI KUU YA VODACOM SEPTEMBER 22

JKT OLJORO Vs POLISI MOROGORO, SH. Amri Abeid

COASTAL UNION Vs TOTO AFRICANS, Mkwakwani


SIMBA SC Vs RUVU SHOOTING

Ukuta uliokuwa unaonekana mwepesi kumenyeka katika michezo ya kirafiki utakuwa na kibarua cha kuendeleza kutoruhusu washambuliaji kuupenya hapo jumapili katika uwanja wa Taifa watakapo wakabili Ruvu Shooting.

Simba SC watakuwa na dhamira ya kuendeleza ushindi hapo jumapili watakapo shuka bila ya nyota wake toka Uganda Emanuel Okwi.


MICHEZO MINGINE YA VPL JUMAPILI

MGAMBO JKT Vs KAGERA SUGAR, Mkwakwani

AFRICAN LYON Vs T.PRISONS, Uwanja wa Azam

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.