KALLY; TUMEPATA DVD ZAO NA TUMEZIFANYIA KAZI

Kocha msaidizi wa azam fc, Kally Ongala leo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa kombe la shirikisho, amebainisha kuwa wamepata DVD ya michezo mitatu ya AS FAR RABAT, wakati wa kocha wa AS FAR RABAT akibainisha yakuwa hawaifahamu azam fc.

Ongala amesema wamepata DVD za mechi tatu za mwisho za AS FAR Rabat, moja ikiwa dhidi ya timu ya Al Nasir ya Libya ambayo waliitoa katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na nyingine mbili za ligi ya Morocco ambazo wanazifanyia kazi kuhakikisha wanashinda kesho.

Naye Ouadani amesema hawaifahamu vizuri Azam, lakini wanaujua mpira wa Tanzania baada ya kuangalia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco uliochezwa machi 23 mwaka huu na kumalizika kwa Tanzania kuibuka na ushindi wa goli 3-1.

Kesho saa 10 alasiri azam fc watawakaribisha AS FAR Rabat katika mchezo wa awali wa raundi ya pili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

AS FAR Rabat inawachezaji 6 katika kikosi cha Moroco kilichopokea kichapo cha goli 3-1 toka kwa Tanzania, wakati azam fc wakiwa na wachezaji wa 5 katika kikosi hicho cha Tanzania lakini alibahatika kucheza ni mmoja kiungo mchezeshaji Salum Aboubakary 'Sure Boy'.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.