vilabu

HALL AIHOFIA SIMBA SC



Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama hadi Desemba 12 kupisha maandalizi ya mechi za Taifa Stars dhidi ya Algeria, lakini benchi la ufundi la Azam FC limeanza kuihofia Simba kuelekea mechi yao inayofuata ya ligi hiyo.

Stewart Hall, kocha mkuu wa Azam, ameweka wazi kuwa ana hofu juu ya mechi hiyo licha ya kikosi chake kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa sasa.

Katika mahojiano na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Hall alisema amejipanga kuhakikisha timu yake inaendelea kuongoza ligi hadi mzunguko wa kwanza utakapokamilika, lakini mchezo dhidi ya Simba unampa wasiwasi ya kuvurugika kwa mipango yake.

"Ni mchezo ambao utakuwa na upinzani mkubwa, ukiangalia kwa sasa Simba si timu ya kuibeza, tuna kazi kubwa mbele yao ili tuendelee kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi," alisema Hall.

"Ninaona Simba ni timu iliyoimarika ukilinginisha ilivyokuwa msimu mmoja au miwili iliyopita, ndiyo maana ninakuambia kutakuwa na upinzani mkali kwenye mechi hiyo," alisemja zaidi Muingereza huyo.

Azam, mabingwa wa Bara 2013/14, watakuwa wenyeji wa Simba katika mechi ya raundi ya 11 ya ligi ya Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 12 huku Wanalambalamba wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa 2-1 katika mechi yao ya mwisho msimu uliopita.

Kikosi cha Hall kiko kileleni mwa msimamo kikiwa na pointi 25 baada ya mechi tisa, pointi 2 mbele ya Yanga katika nafasi ya pili na nne mbele ya Simba walioko nafasi ya nne.

CHANZO: NIPASHE

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.