riadha

ALLIANCE SPORT WANGARA RIADHA

WATOTO wa kike wenye umri mdogo kutoka Shule ya Alliance Sports Academy ya Mwanza, Sara Joel, Filomena Magige na Rehama John, wameonesha uwezo mkubwa katika mashindano ya Taifa ya Riadha katika mbio za meta 100 na 400 na kushinda katika hatua za awali kundi la wanawake.

Mashindano hayo yanayoshirikisha mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na kufanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri hapa, yalianza mapema asubuhi jana na yalitarajiwa kufunguliwa rasmi alasiri na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera.

Mashindano hayo ambayo yameonesha kuwa na ushindani mkali kutoka kwa wanamichezo wa mikoa inayoshiriki, Mwanza umewashirikisha vijana wenye umri ndogo wakiwemo wanafunzi shule ya michezo.

Lengo ni kuendeleza vipaji vya vijana licha ya kila mkoa kushirikisha vijana wengi katika kinyang’anyiro hicho kuwania medali za aina mbalimbali.

Katika kundi la tano, wanawake mbio za meta 100, Rehama alishika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Mariam John kutoka Shinyanga wakati Asha Madoti akinyakua nafasi ya tatu na hivyo kujiweka katika matumaini ya kuingia hatua ya fainali za mbio hizo.

Kundi la kwanza upande wa wanawake mbio za meta 100, mshindi ni Shuwena Ally kutoka Kaskazini Pemba, Sada Juma wa Mbeya na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Anna Yohana kutoka Dodoma.

Wengine walioibuka kidedea katika hatua za awali kutoka kundi pili na mikoa yao kwenye mabano ni Miria Sorri (Pwani), Husna Salim (Dar) na Kazija Hassan (Kusini Pemba).

Pia katika hatua hiyo iliyokuwa na ushindani mkali, washindi wa kundi la tatu, mshindi wa kwanza alikuwa ni Aghata Paul (Tabora), Rebeca Kashinje (Pwani) na Adelina Trazius (Dar), wakati kundi la nne mshindi wa kwanza alikuwa ni Jane Maige (Mara), Subira Hamad (Kaskazini Unguja).

Katika mbio za meta 400 wanawake hatua za awali, kundi la kwanza walioshinda nafasi tatu za juu ni Asha Kuduga (Mtwara), Yenida Paulo (Shinyanga) na Sara Stephen (Tabora).

Wengine walioshinda hatua hiyo kutika kundi la pili la mbio za meta 400 wanawake ni Rose Seif (Pwani), Haimidia Omary (Mjini Magharibi) na Hafisa Mbua (Singida).

Pamoja na kundi hilo, jingine la tatu ambalo miongoni mwao walikuwemo vijana wadogo wawili kutoka Mwanza wakishikilia nafazi ya kwanza na ya pili, wakati tatu ilishikwa na Shuena kutoka Kaskazini Pemba.


Njazo: HABARI LEO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.