VPL

AZAM,YANGA, SIMBA NA COASTAL WOTE SAWA, WAKIIWA NYUMA YA JKT RUVU

Magoli ya Jerry Santo, Didier Kavumbagu, Haruna Chanongwa, Gaudence Mwaikimba na Abdallah Seif zimepelekea timu za SImba, Yanga, Azam na Coastal wanao tazamiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara wakifikisha point 4. Huku wakiwa nyuma ya JKT Ruvu wanye point 6.

UWANJA WATAIFA.


Katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam kulikuwa na mchezo baina ya YAnga na Coastal union mchezo ulio malizika kwa sre ya goli 1-1 huku kukishuhudia kadi nyingi zikitolewa katika mchezo huo.

Ndani ya dakika 45 za kwanza hakukuwa na timu iliyokuwa imeona nyavu za mwenzake huku mchezo ukiwa umebalamce na kukiwa na kila dalili ya mchezo huo kwisha kwa sare tasa.

Katika kipindi cha pili ndipo zahama za kadi zilipoanza na kushuhudia magoli yote mawili yaliyo patikana katika uwanja huo wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Didier Kavumbagu katika dakika ya 69 kabla ya Jerry Santos kuisawazishia Coastal Union katika dakika ya 90 kupitia kwa mkwaju wa penati baada ya kiungo Haruna Niyonzima kuunawa katika eneo la hatari.



UWANJA WA CCM ALLY HASSAN MWINYI, TABORA

Na Msuni Mwemezi

Magoli ya Gaudence Mwaikimba na Abdallah Seif Karinhe hii leo yameipatia Azam FC point Tatu na kuwafanya wa pande mpaka katika nafaci ya 3 wakilingana point na YAnga, coastal union na Simba SC wakipishana katika uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Azam FC leo walikuwa katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora wakiwa wamekaribishwa na wanajeshi Rhino Ranger ya mkoani hapo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Azam FC waliutawala mchezo huo na dalili ya ushindi zilianza kuonekana mapema baada ya Kippre Tchetche na Khamisi Mcha kupoteza nafasi kadhaa katika kipindi hicho cha kwanza.

Kocha Stewart Hall alilazimika kufanya mabadiliko asiyo ya kusudia baada ya mshambuliaji Kipre Herman Tchetche kuumia na nafasi yake kujazwa vyema Abdallah Seif Karinhe katika kipindi hicho cha kwanza.

Azam FC waliandika goli lake la kwanza kwa shuti kali la Gaudence Mwaikimba katika dakika 55 baada ya dakika 45 za mqwanzo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kuingia kwa goli hilo liliwaduliza wachezaji wa Azam FC waliokuwa wanasaka goli la kuongoza kwa udi na uvumba na kuanza kuwapa burudani mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo huku wakiwa wanasaka goli la pili.

Kijani aliyekulia katika kituo cha Orange Academy kilichopo Zanzibar kabla ya kujiunga na academy ya Azam FC Abdallah Seif Karinhe kuandika goli la pili kwa Azam FC katika dakika ya 79 na kupelekea Azam FC kutoka ,bele kwa goli 2-0.


UWANJA WA SHEKHE AMRI, ARUSHA

Simba SC leo wamefanikiwa kupata point tatu mbele ya JKT Oljoro katika uwanja huo baada ya kuondoka na ushindi wa goli 1-0.

Goli pekee la Simba SC lililo pelekea Imba kufikisha point 4 sawa na Yanga, Azam na Coastal Union lilifungwa na mshambuliaji chipukizi wa Haruna Chanongo katika dakika ya 33.


MATOKEO MENGINE

MBEYA CITY 2-1 RUVU SHOOTING
JKT RUVU 3-0 PRISONS
MGAMBO SHOOTING 1-0 ASHANTI UNITED
MTIBWA SUGAR 1-0 KAGERA SUGAR

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.