wachezaji

BABI ANAMATUMAINI YA KUREJEA VETNAM

Kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Yanga na Azam FC, Abdi Kassim "Babi" anajianda kurejea nchini Vetnam baada ya kuto ongezewa mkataba na timu aliyokuwa anaitumikia msimu uliopita Azam FC.

Babi amesema kuwa yuko mbioni kurejea Vetnam hapo mwakani baada ya kuwa nchini humo kwa takribani mwaka mmoja kabla yua kujiunga na Azam FC, akiwa anaitumikia klabu ya DT long ya nchini humo.

Babi ameyazungumza hayo baada ya kuonekana akifanya mazoezi na timu ya KMKM inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar na inanolewa na kocha aliyekuwa msaaidizi wa Mbrazili Marcio Maximo katika timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", Ally Bushiri.

Akizungumzia hali ya kufanya mazoezi na KMKM kiungo huyo aliyefunga goli la kwanza katika uwanja wa taifa kwa shuti la mbali pale Taifa stars walipo wachapa goli 1-0 Uganda katika mchezo wa kirafiki uliokuwa mchezo wa kwanza kuchezwa katika uwanja huo amesema kuwa, amesaini kuitumikia KMKM katika msimu ujao wa ligi kuu ya Zanzibar inayo dhaminiwa na Grand Malt.

Babi amesema kuwa ataitumikia KMKM mpaka pale safari yake ya kurejea Vetnam itakapo iva kwakuwa bado ana ndoto ya kutoka nnje ya TAnzania kwa mara nyingine Tena.

KMKM ikiwa jnajiandaa na ligi kuu ya Zanzibar na mashindano ya kimataifa wamemuongeza pia katika kikosi chao mshambuliaji Ahmed Shibolo.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.