kitaa

KITAANI: COASTAL WAPIGWA MAWE

kUTOKA KWENYE FACEBOOK PAGE YA  Coastal Union
Mbali ya mwamuzi kufanya kisichotarajiwa kwa timu zote mbili lakini mashabiki wa Yanga bado walishikilia kuwa Coastal Union wamebebwa hata kuzawadiwa penalt dakika ya 90 na nahodha Jerry Santo kutumbukiza wavuni na kugeuza matokeo kuwa 1-1. Hata hivyo gari la wachezaji wa Coastal Union lilishambuliwa na mashabiki wa Yanga hata kuvunjwa kioo cha pembeni na beki wa Coastal Union Hamad Juma kupasuliwa sehemu ya kichwa akashonwa nyuzi kadhaa. Viongozi wa Coastal Union wanauliza je huu ni uungwana?
Photo
Hii ndiyo siti aliyokaa Hamad Juma beki wa Wagosi wa kaya hata kupasuliwa na jiwe sehemu ya kichwani.

About kj

1 comments:

Anonymous said...

Washabiki wa hawajitambui. Kama kuna tukio baya linalostahili kulaaniwa na wapenda michezo ni hili la kuwashambulia kwa mawe Wachezaji na viongozi wa Coastal Union. Yanga wajue kuwa zama za kuwa watawala wa milele wa soka la Tanzania wao na mahasimu wao Simba zinakaribia mwisho. Timu kama Coastal, Azam na Kagera Sugar zitaleta mapinduzi mapya. Kuwa na wingi wa washabiki hakusaidii kama mashabiki wenyewe hawajui maana ya mpira.
Hata hivyo, haitashangaza kusikia kuwa suala hili litafumbiwa macho na kuachwa likipita hivi hivi.
Huu ni mchezo wa kwanza, Yanga nao watakwenda Tanga; je wanategemea nini kutoka kwa washabiki wa soka wa Coastal na mkoa wa Tanga kwa ujumla?

Powered by Blogger.