riadha

RIADHA ARUSHA KUELEKEA MORO

Na Athumani Issa, Moshi: TANZANIA DAIMA

TIMU ya riadha ya Mkoa wa Arusha inatarajiwa kuondoka jijini humo kesho kwenda Morogoro kwenye mashindano ya Taifa yatakayofanyika Agosti 23 na 24 kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Kwa mujibu wa Kocha wa timu hiyo, Felix Chunga, alisema kikosi chake kinaundwa na wanariadha wanane wanaume na watatu wanawake.

Chunga aliwataja wanariadha wanaounda kikosi chake kuwa ni Laurent Masatu (mita 100, 200), Baraka Hamis (mita 400), Michael Nkungu (mita 800, 1,500), kutoka JWTZ, Thobias Bura (mita 1,500), Joseph Theophil (mita 5,000), kutoka Team 100, Said Thomas (mkuki/tufe), Tony Credo wa JWTZ, na Omary Mbaraka (100x4).

Kocha huyo aliwataja kwa upande wa wanawake kuwa ni Jacqueline Sakilu kutoka JWTZ, Teoflasia Sumaye (mita 5,000), na Rosalia Fabian (mita 1,500).

Chunga aliongeza kuwa vijana wake wamejiandaa vema na ana uhakika kutoa ushindani mkubwa.
Mabingwa wa taifa wa riadha mwaka jana ni Mkoa wa Mjini Magharibi huku Arusha ikikamata nafasi ya pili.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.