simba

SIMBA WABANWA KWA MWINYI

Mnyama Simba leo wameshindwa kutamba katika uwanja Alihasan Mwinyi mkoani Tabora baada ya kulazimishwa sare ya goli 2-2 na wanajeshi wa Rhino Rangers ya Tabora.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom uliochelewa kuanza leo kutokana na wachezaji wa Rhino Ranger kutokuwa na leseni kitendo ambacho ni kinyume na kanuni.

Mchezo huo ulianza baada ya Simba kuhakikishiwa leseni za wachezaji wa Rhino Rangers zitatumwa kwa njia ya barua pepe na mpaka mapumziko zingekuwa zimeshafika.

Simba walikuwa wa kwanza kupata goli katika daika ya 4 kupiti kwa Jonas Mkude kabla ya Rhino Rangers kusawazisha na Simba SC kupata goli la pili na kupelekea mchezo kwenda mapumziko simba wakiwa mbele kwa goli 2-1.

Rhino Rangers wanao shiriki ligi kuu ya vodacom kwa mara ya kwanza wakiwa wameirejesha ligi hiyo Mkoani Tabora toka Milambo ishuke daraja walisawazisha doli hilo katika kipindi cha pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa sre ya goli 2-2.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.