Wanariadha
wa Polisi Tanzania walioshika nafasi ya kwanza mpaka ya tano katika
mbio za Km 12 (Cross Counrty) pamoja na mwalimu wao Naasi Gwagwe wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mbio hizo katika chuo cha
Polisi Nchini Namibia wakati wa Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa
Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Wanariadha
wa Polisi Tanzania walioshika nafasi ya kwanza mpaka ya tano katika
mbio za Km 12 Cross Counrty (walioshika bendera) wakiwa katika picha ya
pamoja na washabiki wao baada ya kumaliza mbio hizo katika chuo cha
Polisi Nchini Namibia wakati wa Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa
Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO).(Picha na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia).
Hatimaye
Michezo ya nane ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa
Afrika (SARPCCO) inatarajiwa kufikia kilele chake kesho huku Wanariadha
wa Tanzania wakihitimisha kwa kishindo baada ya kutawala mbio za KM 12
(Cross country) kwa kunyakua nafasi ya kwanza hadi ya tano.
Wanaridha
waliofanya vyema na nafasi zao katika mabano ni pamoja Fabian Nelson
(1) muda wa dakika 35:36:20 ,Basil John (2), muda wa dakika
35:38:81,Silvester Simon (30) muda wa dakika 36:42:56,Wilbaldo Peter (4)
muda wa dakika 36:48:22, na Osward Revelian (5) muda wa dakika 37:36:20
Kwa
matokeo hayo mpaka sasa Polisi Tanzania imefikisha jumla medali 15,huku
Dhahabu 6,Fedha 4,Shaba 5 ambapo katika ufungaji hapo kesho medali
zinatarajiwa kuongezeka kutokana na kuwa na wanariadha wengi waliofanya
vizuri pamoja na matokeo katika mchezo wa vishale(dats).
Kwa
upande wa Mpira wa miguu, timu ya Polisi Tanzania imeishia katika hatua
ya robo fainali baada ya kukubali kichapo cha magoli 2 kwa 1 dhidi ya
Afrika Kusini hivyo fainali itachezwa kati ya Afrika Kusini na Zimbabwe
huku mpira wa miguu kwa wanawake fainali itachezwa kati ya Kongo na
Angola.
Mpira
wa pete timu ya Polisi Tanzania imeshika nafasi tano huku Polisi
Swaziland ikishika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Zimbabwe, Zambia na
Afrika kusini.
Kwa
mujibu wa Mwalimu wa Riadha Polisi Tanzania Naasi Gwagwe wanamichezo wa
riadha wamefanya vizuri kutokana na kuzingatia mazoezi hasa wakati wa
kambi yao waliyokuwa wameiweka katika chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi
(MPA) kwa kipindi cha mwezi mmoja.
0 comments:
Post a Comment