riadha

WANARIADHA WAZOA MEDALI SARPCCO

Na Frank Geofray, TANZANIA DAIMA

WANARIADHA wanaowakilisha Jeshi la Polisi Tanzania katika michezo ya Umoja wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO), jijini hapa, wameanza vema mbio hizo baada ya kufanikiwa kunyakua medali za dhahabu na fedha katika mbio za mita 10,000 wanaume.

Aliyenyakua medali ya dhahabu ni Fabian Nelson aliyetumia dakika 30:42 na kufuatiwa na Wilbrado Peter pia wa Tanzania aliyetumia dakika 30:45 na kuwaacha wanariadha kutoka Zimbabwe, Namibia, Botswana na Angola.

Wengine walioipa Tanzania medali ni pamoja na Basil John mita 800 aliyetwaa shaba na Mohamed Ibrahim kurusha kisahani aliyetwaa naye shaba.

Katika soka, mechi ya ufunguzi iliwakutanisha wenyeji Namibia na Msumbiji, ambapo wanyeji walishinda mabao 2-0 huku soka kwa wanawake, Namibia na Angola zilikwenda sare ya bila kufungana.

Tanzania itaanza kutupa karata yake katika soka dhidi ya Zambia, ambapo imepangwa kundi B pamoja na timu za Zambia, Angola, DRC na Lesotho huku Kundi B lina Namibia, Msumbiji, Botswana na Zimbabwe.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.