VPL

YANGA WAPELEKA ZAAMA NZITO KWA WAUZA MITUMBA

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wamepeleka zaama nzito kwa wauza mitumba wa Ilala Ashanti United baada ya kuwachapa goli 5-1 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa hii leo.

Yanga walinza kuandika magoli yao kupitia kwa Jerry Tegete katika dakika ya 10, goli lililo dumu mpaka mapumziko, lakini hali ikawa tofauti katika kipindi cha pili kufuatia goli Saiman Msuva katika dakiak ya 48.

Goli hilo la pili lilizidisha hamu kwa yanga ya kutaka magoli zaidi na katka dakika ya 58 alikuwa Jerry Tegete alieandika goli la tatu la Yanga kabla ya kiungo toka Rwanda Haruna Niyonzima kuandika goli la 4 katika dakika ya 74.

Wakati mchezo ukielekea mwishoni Ashanti United waliandika goli lao la kufutia machozi kupitia kwa Shabani Juma katika dakika ya 90.

Alikuwa kiungo wazamani wa Moro united na Mtibwa sugar Nizar Kharfan aliyehitimisha kalamu ya magoli kwa Yanga katika dakika ya nyongeza na kuwatoa Yanga kifua mbele kwa goli 5-1.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.