vilabu

NAMNA MBEYA CITY WALIMVYOWAFANYIA FUJO PRISONS

 Taarifa kutoka mjini Mbeya zinaeleza mashabiki wa Mbeya City wamelishambulia gari la wachezaji wa Prisons na kumuumiza mchezaji mmoja.
Pamoja na kumuumiza mchezaji huyo, mashabiki hao pia walivunja vioo vya  gari aina Toyota Coaster na magari mengine yalipokuwa kwenye msafara wa timu hiyo ikitoka uwanjani baada ya kufungwa na Mbeya City kwa mabao 2-0.

Mashabiki hao walilishambulia magari hayo na kuyavunja vioo na baada ya hapo wakakimbilia kusikojulikana.

Mmoja wa maofisa wa Prisons alisema ana uhakika kuwa waliofanya hivyo ni mashabiki wa Mbeya City kwa kuwa walikuwa wamevaa jezi za rangi ya zambarau ambayo huvaliwa na timu hiyo.







PICHA NA MBEYA YETU BLOG

About Unknown

1 comments:

Anonymous said...

polisi kwann hawatoi escort kwa timu zinapoondoka uwanjani mikoani, au taifa tu Simba na Yanga ndo wakusindikizwa

Powered by Blogger.