gofu

NMB KUDHAMINI GOFU YA NYERERE

Na  Clezencia Tryphone: TANZANIA DAIMA 

BENKI ya NMB, imejitosa kudhamini mashindano ya gofu kuadhimisha miaka 14 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, yatakayofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea udhamini huo wa sh milioni 17.3 jana, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Joseph Tango, aliishukuru benki hiyo kwa kujitosa kudhamini mchezo huo katika kuadhimisha siku hiyo ya kitaifa.

Alisema mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kesho hadi Oktoba 14, ambako zaidi ya wachezaji 152 watashiriki kutoka Tanzania Bara na Visiwani, ambako pia timu ya taifa ya mchezo huo itashiriki ili kujiandaa na mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Nairobi Kenya hivi karibuni.

Naye Mkuu wa Masoko wa NMB, Richard Makungwa alisema wamevutiwa kudhamini shindano hilo kwa lengo la kuona mchezo huo ukifanya vema, hasa ikizingatiwa benki yao imegawanyika na kuwafikia Watanzania wengi hapa nchini.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.