netball

Mh. ABOOD ATAKA NETBALL MASHULENI


MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood, amevishauri vyama vya netiboli Taifa, wilayani na mikoani, kuelekeza nguvu mitaani na shuleni katika kuhamasisha mchezo huo ili uendelezwe kwa kupata timu nyingi zaidi zitakazoshiriki mashindano ya ligi ya ngazi mbalimbali, hivyo kuinua mchezo huo.

Abood alisema hayo kwenye hotuba yake ya ufungaji wa mashindano ya Ligi Kuu ya Muungano iliyoanza tangu Septemba 3 na kufikia tamati juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri, ikishirikisha timu nane zikiwamo tatu za Zanzibar.

JKT Mbweli ilifanikiwa kutetea taji hilo baada ya kulitwaa kwa mara ya pili mfululizo. Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo hilo, kuwepo kwa Ligi Kuu ya Muungano, kunadhihirisha namna Watanzania wanavyouenzi Muungano uliopo hasa kwa nyakati za hivi sasa, wakati wa mchakato wa Katiba mpya.

“Nimefurahishwa mashindano haya makubwa yenye sura ya Muungano wetu kufanyika hapa Morogoro...yanaimarisha udugu wetu na umoja wetu ulioasisiwa na waasisi wetu, Mzee Karume na Mwalimu Nyerere,” alisema Abood.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa Chaneta na Chaneza kuwa mashindano ya Ligi Kuu ya Muungano ya mwaka ujao yafanyike tena Morogoro na yenye atahakikisha yanaboreka zaidi tofauti na mwaka huu.

“Nikiwa mbunge mwenyeji, nitawashawishi wabunge wenzangu wa mkoa huu wachangie kufanikisha mashindano haya ambayo ndiyo pekee yanadumisha Muungano wetu,” alisema Abood.

Awali, Mwenyekiti wa Chaneta, Anne Kibira, licha ya kutaja changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa ufadhili, pia alizipongeza timu zilizoshiriki ambazo zote ni za majeshi sambamba na viongozi wao kwa kutambua suala la kukuza na kuimalisha michezo ukiwemo wa netiboli.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.