TIMU ya netiboli ya Halmashauri ya wilaya ya Njombe katika mkoa mpya wa Njombe , imejipatia ushindi mnono dhidi ya wapinzani wake timu ya Halmashauri ya wilaya ya Lushoto kwa kuifunga mabao 55-13.
Pamoja na timu ya Halmashauri ya wilaya ya Lushoto kushangiliwa kwa nguvu na wenzao, haikufua dafu mbele ya wachezaji wa timu ya wilaya ya Njombe kwani hadi mapunziko ilikuwa mbele kwa mabao 27-6 .
Mchezo huo ulifanyika asubuhi ya jana katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa sambamba na mechi nyingine za mchezo huo kwenye mashindano ya Shimisemita 2014.
Pamoja na mchezo huo, mwingine uliokuwa wa kuvutia ni kati ya Halmashauri ya wilaya ya Arusha dhidi ya majirani zao Halmashauri ya wilaya ya Moshi, ambapo Arusha iliifunga Moshi kwa mabao 34-19, hadi mapumziko Arusha ikiongoza kwa mabao 12-11.
Mbali na mchezo huo, pia timu ya Halmashauri ya Jiji la Arusha iliifunga timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hanang kwa mabao 37-24, wakati Halmashauri ya wilaya ya Mpanda iliifunga Halmashauri ya wilaya ya Mvomero kwa mabao 30-20.
Wakati timu ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa iliishinda Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu mabao 15-14 na timu ya Halmashauri ya wilaya ya Kwimba iliifunga Halmashauri ya wilaya ya Kilombero mabao 26-18.
Katika mchezo mwingine uliofanyika jana asubuhi uliokuwa wa vuta ni kuvute ulizikutanisha kati ya timu za Halmashauri ya wilaya ya Mbozi na Halmashauri ya mji Mpanda. Timu hizo hadi mapumziko zilitoa sare ya kufungana mabao 9-9.
CHANZO: HABARI LEO
Pamoja na timu ya Halmashauri ya wilaya ya Lushoto kushangiliwa kwa nguvu na wenzao, haikufua dafu mbele ya wachezaji wa timu ya wilaya ya Njombe kwani hadi mapunziko ilikuwa mbele kwa mabao 27-6 .
Mchezo huo ulifanyika asubuhi ya jana katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa sambamba na mechi nyingine za mchezo huo kwenye mashindano ya Shimisemita 2014.
Pamoja na mchezo huo, mwingine uliokuwa wa kuvutia ni kati ya Halmashauri ya wilaya ya Arusha dhidi ya majirani zao Halmashauri ya wilaya ya Moshi, ambapo Arusha iliifunga Moshi kwa mabao 34-19, hadi mapumziko Arusha ikiongoza kwa mabao 12-11.
Wakati timu ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa iliishinda Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu mabao 15-14 na timu ya Halmashauri ya wilaya ya Kwimba iliifunga Halmashauri ya wilaya ya Kilombero mabao 26-18.
Katika mchezo mwingine uliofanyika jana asubuhi uliokuwa wa vuta ni kuvute ulizikutanisha kati ya timu za Halmashauri ya wilaya ya Mbozi na Halmashauri ya mji Mpanda. Timu hizo hadi mapumziko zilitoa sare ya kufungana mabao 9-9.
CHANZO: HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment