TIMU sita za netiboli zilizokuwa
zinashiriki fainali za Ligi Daraja la Pili Taifa zilizomalizika jijini
Tanga, zimepanda daraja, imeelezwa. Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli
Tanzania (Chaneta), Annie Kibira alisema timu hizo zitachukua nafasi ya
timu sita zilizoshushwa daraja kutoka katika Ligi Daraja la Kwanza.
Kibira alizitaja timu zilizopanda daraja
kuwa ni Magereza, Chuo cha Dar es Salaam, Sedico ya Mwanza, Halmashauri
ya Jiji la Tanga, Lindi Queens ya Lindi, Kigoma Queens ya Kigoma na
Korogwe Queens ya Tanga.
Wakati timu zilizoshuka daraja kwa
sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza bila
kutoa sababu ni Polisi Mbeya, mabingwa wa zamani Filbert Bayi,
Magereza, Tumaini na Teachers Kinondoni.
Akizungumzia mashindano ya Ligi Daraja
la Pili yaliyomalizika Tanga, Kibira alisema yalikuwa na msisimko wa
aina yake ukiondoa kasoro ndogo ndogo za baadhi ya timu kuchelewa kufika
kituoni.
Naye Mwenyekiti wa Filbert Bayi
Foundation (FBF), Filbert Bayi alisema hivi karibuni kuwa kuivunja timu
yao ya netiboli baada ya kubaini kuwa uongozi wa sasa wa Chaneta hauna
nia ya kuuendeleza mchezo huo kimataifa baada ya kushindwa kushiriki
mashindano yoyote ya kimataifa tangu uingie madarakani.
Alisema wao walianzisha timu hiyo kwa
lengo la kuinua vipaji vya wachezaji kitaifa na kimataifa, lakini
Chaneta imeshindwa kuipeleka timu katika mashindano yoyote ya kimataifa.
Chaneta imedai ukata umefanya ishindwe
kuipeleka Taifa Queens katika mashindano ya mataifa Singapore, ya Afrika
Malawi, mashindano ya vijana Botswana na ya kufuzu kucheza Kombe la
Dunia yaliyofanyika Gaborone hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment