judo

25 KUUNDA TIMU YA TAIFA YA JUDO

KOCHA wa timu ya Taifa ya Judo, Zaidi Khamis ametaja kikosi cha wachezaji 25 walioanza kambi ya kujiandaa na mashindano ya Kanda ya Tano yatakayofanyika Januari mwakani.

Wachezaji hao ni washindi wa mashindano ya taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki ambapo yalilenga kuchagua kikosi hicho ili kuanza maandalizi ya michuano hiyo ya kimataifa.

Waliochaguliwa ni Ahmed Magogo kilo 60, Abuu Mcheteko (60), Salmin Bunu (60), Philipo Sabini (66), Omar Uledi (66), Emmanuel Mkande (66), Moses Matulanda (66), Rahimu Ally (66), Andrew Mlugu (73), Mohamed Kisandu (73), Seif Malulu (73) na Lucas Shirima (73).

Wengine ni Mohamed Korogombe (81), Gervas Chilipweli (81), Jeremia Makame (81), Rajabu Chuhila (81), Geoffrey Mtawa (90), Mussa Kagoma (90), Kusekwa Izengo (90), Augustino Simbili (90) na kwa upande wa wanawake ni Matilda Temba, Pilly Mohamed, Diana Marcus, Paulina Mbezi na Marry Awedasia.
Katibu Mkuu wa Chama cha Judo, Innocent Mallya alisema jana kuwa tayari kikosi hicho kimeshaanza kambi kuanzia jana katika mazoezi wanayofanya kwenye ukumbi wa Kisutu, Dar es Salaam.

Mallya alisema sababu ya kuweka kambi mapema ni kwa sababu wamedhamiria kutetea ubingwa wanaoushikilia. Timu hiyo ndio mabingwa mara mbili wa mwaka 2013 na mwaka huu, hivyo katika michuano ya mwakani itakayoandaliwa na Tanzania, wanategemea kutetea ubingwa huo.

Katika mashindano ya Kanda ya Tano yatakayofanyika nchini mwakani, yanatarajia kushirikisha Rwanda, Zanzibar, Burundi, Kenya, Ethiopia na baadhi ya nchi nyingine za Afrika ya Kati ambazo zitapelekewa mialiko.

Mallya alisema washindi watakaofanya vizuri kwa upande wa timu ya Tanzania na ile ya Zanzibar baadaye wataunda timu moja ya muungano kwa ajili ya kujiandaa na Michezo ya Afrika maarufu ‘All African Games.’

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.