vilabu

NDANDA YACHUKUWA MSHAMBULIAJI WA MTIBWA SUGAR

TIMU ya Ndanda FC imemnasa aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Masoud Chile ambapo tayari ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kukisaidia kikosi hicho.

Mchezaji huyo alimaliza mkataba wake dhidi ya Mtibwa msimu uliopita wa mwaka 2013/2014 hivyo alisajiliwa na Ndanda FC juzi kama mchezaji huru.

Akizungumza na gazeti hili jana Msemaji wa Ndanda Idrissa Bandari alisema huyo ni mchezaji wa kwanza bado wanaendelea na mchakato wa kuwapata wengine watano.

“Tumemsainisha mchezaji huyo tunaendelea kuzungumza na wengine wenye uzoefu na soka, tukikubaliana nao tutawasainisha wakati wowote,” alisema Bandari.
Hivi karibuni baada ya ligi kusimama Katibu Mkuu wa Ndanda FC Edmund Kunyengana alisema lazima wafanye usajili katika dirisha hili dogo kwa ajili ya kuhakikisha timu inafanya vizuri.

Dirisha la usajili limefunguliwa tangu Novemba 15 na litafikia tamati Desemba 15 kabla ya ligi kuendelea Desemba 26.

Ndanda FC haijafanya vizuri tangu imeanza Ligi Kuu Tanzania Bara kama ambavyo ilidhamiria awali kwani ilijikuta ikiwa miongoni mwa timu zilizofungwa mabao mengi.

Katika msimamo wa ligi Ndanda inashika nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa ina pointi sita nyuma ya Prisons huku Mbeya City ikishika mkia.

CHANZO: HABARI LEO

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.