Mwaka huu Chaneta imekuwa na wakati mgumu wa kuandaa timu ya taifa kwenye mashindano ya kimataifa sababu ya kukosa udhamini.
Akihojiwa na kituo cha runinga ya taifa cha TBC1 jana Mwenyekiti wa Chaneta Anna Kibira alisema kuwa kutafuta fedha ni jambo muhimu na watalipa kipaumbele katika kufanikisha mipango yao.
“Mkakati wetu wa kwanza ni kutafuta fedha kwasababu ndio kila kitu tutazungumza na wadhamini mbalimbali, kuona kwa vipi watusaidie katika kufanikisha,” alisema.
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilitambua changamoto ambazo Chaneta na baadhi ya vyama vya michezo imekumbana na matatizo kiasi cha kuvisaidia kutafuta udhamini wa Mashindano ya Afrika Mashariki mapema mwaka huu.
Kibira alisema pia wanatarajia kuwaendeleza vijana walioonesha uwezo katika michuano mbalimbali iliyofanyika mwaka huu ikiwemo ile ya Afrika Mashariki kwa Shule za Sekondari (Feasssa).
Alisema michuano hiyo imeonesha wazi kuwa na vipaji vingi ambavyo bado havijapewa nafasi ya kuonesha uwezo wao.
0 comments:
Post a Comment