tenesi

KENYA YAIFUNIKA TANZANIA SIKU YA KWANZA YA DAR OPEN

WACHEZAJI tenisi kutoka Kenya jana walifunika Watanzania katika michuano ya kimataifa ya kwanza ya tenisi kwa walemavu (Dar Open ) iliyoanza na kutarajiwa kuhitimishwa leo katika viwanja vya Gymkhana.

Kwa mujibu wa matokeo ya jana mechi saba zilienda kwa Wakenya kwa nafasi ya wanaume na wanawake na mbili ndio walishinda Watanzania.

Michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO, Merceds- Benz na kampuni ya mawakili ya Dar es Salaam ya IMMMA imelenga pia kuandaa wachezaji kwa ajili ya mechi za kufuzu michezo ya dunia zinazotarajiwa kupigwa Kenya, Februari mwakani.

Kwa mujibu wa msemaji wa wadhamini wa michuano hiyo Alexander Sarac, michuano hiyo yenye washiriki wanaume 17 na wanawake watano kutoka Tanzania na Kenya, imelenga kuwezesha walemavu kuendeleza vipaji vyao vya kucheza tenisi.

Fungua dimba ya michuano hiyo ilianzishwa na watanzania Novatus Temba na Moses Sebastian ambapo Temba alimchapa Sebastian kwa seti 2-0, Mkenya Itaken Timoi alimvuruga Bernad Antony kwa seti 2-0 huku Mkenya mwingine Peter Mnuve akimtoa Mtanzania Albert John kwa seti 2-0.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.