kitaa

KITAANI: NANI WA KUULIZA NA KUJIBU, JUU YA NURDIN NA JEBA

Na Mkubwa Kambi kutoka Kandanda

Katika vitu ninavyoviheshimu ni muendelezo wa habari, yaani napenda sana kinachoandikwa leo tukikimbuke hata mwakani kwa faida ya wote, na kumbukumbu ndio huwa zinatupa somo zuri sana.

Hebu njooni hapa rafiki zangu, hii nchi siku zote huwa ninasema tumelaaniwa kama si kurogwa, mnamkumbuka Nurdin Bakari, yule kiungo bora kabisa aliyepata kuzichezea Simba SC na Yanga?

Unakumbuka mkasa uliomtoa Simba SC na kumpeleka Yanga?

Anyway nitawakumbusha kidogo kuna habari zilienezwa kuwa yule bwana ni mgonjwa wa moyo na hawezi kucheza soka labda akafanyiwe operation!! Sikumbuki ni lini alifanyiwa operation, hatimaye alienda Yanga na akakipiga kwa ufanisi mkubwa tu!!

Mnamkumbuka mchezaji mmoja hivi chipukizi aliyekuwa pale Azam FC almaarufu kama "Jeba"? yule kijana Simba walimtaka kwa udi na uvumba Azam wakaapa na miungu yote kuwa hawezi kwenda Simba kwani nao bado wanamhitaji!!

Unajua kilichoendelea? Hahahahahaha Azam wakamtangaza mchezaji yule kuwa ni mgonjwa wa moyo hawezi tena kucheza soka, yaani kifupi carrier yake ya soka ndio imeishia pale!! Sitaki kupinga hili!!

Juzi nikiwa Dar nilipigiwa simu na bwana mdogo mmoja, akaniambia,'Kaka tumepigwa na Mtibwa Suger 4-2, lakini pale kati kwenye middle ya Mtibwa alikuwepo yule dogo "Jeba" amekichafua mbaya". mwisho wa kunukuu.

Nilijiuliza maswali lukuki kichwani mwangu, huyu "Jeba" amepona ama anaendekeza njaa tu?

Ama ilikuwa mizengwe tu ili asiende Simba?

Nani atanijibu maswali haya? hapa ndipo matatizo yetu ya msingi yanapoanzia, tunatembea na maswali mengi yasiyo na majibu, nani wa kuuliza maswali haya kwa wahusika?

Wanaopaswa kuulizwa maswali haya ni kina nani?

Kwanza Daktari aliyeandika ripoti ya "Jeba" pili "Jeba" mwenyewe, tatu Azam na nne ni Mtibwa.

Nani anayepaswa kuuliza haya maswali? Ni waandishi wa habari "full stop". Hebu tusaidieni kupata ukweli wa habari hizi

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.