kitaa

Video ya Yanga na Zamalek pamoja na maneno ya mpinzani



Kitaa kimetua katika mtaa wa Mjengwa Blog na kukutana na maneno ya mtani wa bingwa wa Tanzania Bara Yanga baada ya sare ya goli 1-1.

TWENDE KITAANI

Simba wenzangu,

Watani zetu Yanga ni watu wa ajabu sana. Wao wanadhani mpira unachezewa Clouds FM na TBC1!

Halafu katika wote, sikudhani kocha wa Yanga angefikiria kumpanga Chuji na Nsajigwa kwenye mechi yao ya leo na Zamalek. Hovyo kabisa.

Na pale kati kati Nyonzima alikuwa peke yake wakati Zamalek walijaza viungo na hivyo kupanga mawe.

Yanga washukuru Zamalek waliamua kujihami zaidi. Kwao Misri, Yanga wategemee kipigo cha bao zaidi ya tatu.

Hata hivyo, Misri ni nchi nzuri ya kufanya utalii. Watani zetu Yanga, e nendeni mkatalii

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.