Usajili wa ligi kuu ya Tanzania bara
inayodhaminiwa na vodacom, ulifungwa jana saa sita usiku huku
kukishuhudia wachezaji mbalimbali wakiachwa na wengine wakitoka
katika timu moja kwenda timu nyingine.
Sports In Bongo leo inakuletea matukio
katika mfumo wa namba, yaliyojitokeza katika dirisha hili dogo la
usajili.
0. IDADI YA MECHI ZA USHINDANI ZA DIARA
Kiungo raia wa Mali, Ismaili Diara
aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu na mabingwa wa Tanzania bara
baada ya kufanya majaribio na kufuzu, na katika dirisha hili ndogo
jina lake limeondolewa katika usajili wa Azam FC bila ya kucheza
mchezo hata mmoja wa mashindano.
Diara akiwa Azam Fcsamepata kucheza
michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimuu huu wa ligi kuu ya
Tanzania bara, na kushindwa kupenya kwenye kikosi cha azam FC mara
baada ya ligi kuuanza na kukosa nafasi ya hata kukaa kwenye benchi la
Azam FC katika michezo yote saba ya ligi kuu iliyochezwa mpaka sasa.
Nafasi ya Diara imechukuliwa na Muivory
coast Pascal Wawa amabaye ni mlinzi wa kati.
1. EMERSON NA JAJA
Inakwenda kwa Wabrazili wa wili ambao
wAmeondolewa katika kikosi cha yanga kwa sababu mbalimbali. Wabrazili
hao ni Jaja na Emerson ambao wote walikuja nnchini kwa nyakati
tofauti kuitumikia yanga sc.
Jaja alisajiliwa na yanga mwanzoni mwa
msimu na kufanya vyema katika michezo ya kirafiki ambapo kila mchezo
ambao yanga ilifunga goli lazima jina la Jaja liwemo, ila mambo
yalikwenda vyongo katika ligi kuu, kwani ndanoi ya mechi 7 ameshinda
goli 1 tu.
Jaja alisoma alama za nyakati na
kuombwa mkataba wake usitishwe katika dirisha hili dogo na nafasi
yake ikajazwa na kiungo toka Brazili Emerson ambaye nae ameshindwa
ameshindwa kufikisha mwezi ndani ya yanga toka asaini mkataba wa
mwaka mmoja.
Emerson amecheza mchezo mmoja tu wa
kirafiki dhidi ya Simba SC kabla ya jana mkataba wake kusitishwa na
kuchukuliwa mshambuliaji toka Burundi hamisi ambwe ndani ya anga.
2. WACHEZAJI WALIOSIMAMISHWA WAPELEKWA KWA MKOPO
Dirisha hili dogo limeshuhudia
wachezaji wa wili waliokuwa wamesimamishwa na uongozi wa Simba SC
Amiri Kiemba na aruna Chanongo wakitolewa kwa mkopo kwenda Azam FC na
Stand united.
Amir Kiemba ameenda kwa mkopo Azam FC
wakati Chanongo akitua Stand United kwa mkopo baada ya kutuumiwa
kuhusika na matokeo mabovu ya Simba SC katika michezo minne ya awali
ambayo Simba SC waliambulia sare.
3. VIPIMO VYA AFYA
Katika dirisha hili dogo la usajili
tumeshuhudia kwa mara ya kwanza wachezaji wakifanyiwa vipimo vya afya
kabla ya kusaini mkataba na klabu husika, ila si wachezaji wote
waliosajiliwa ndio waliofanyiwa vipimo vya afya katika dirisha hili
dogo la usajili bali ni wachezaji watatu tu ndio waliopitia katika
vipimo vya afya nao ni Pascal Wawa aliyejiunga na Azam FC, Danny
Ssenkuruma aliyejiunga na Simba SC na Kpah Sherman aliyejiunga na
yanga.
4. INGIZO JIPYA LA WAGANDA
Dirisha hili dogo la usajili
limeshuhudia ingizo la wachezaji 6 wakigeni kati yao nne ni raia wa
Uganda, ambao wamejiunga na klabu ya Simba SC na Azam FC.
Wachezaji wengine ni kutoka Liberia
ambaye ni Sherman aliyejiunga na anga na Muivory coast Wawa
aliyejiunga na Azam FC.
Waganda hao wapya ni Saimon na Danny
Sserkuma, Juuko Murshid waliojiunga na Simba SC na Brian Majegwa
aliyejiunga na Azam FC.
5. IDADI YA WAGANDA
Baada ya Simba SC kuingiza wachezaji wa
tatu toka Uganda na kupelekea kuwa na wachezaji watano wa toka Uganda
katika kuhitimisha kwa ligi kuu ya msimu huu, kitendo ambacho
kinaweza kikawa ni rekodi kwa klabu ya Simba SC kuwa na wachezaji
wote wakigeni toka taifa moja.
Simba SC ina waganda Emanuel Okwi,
Joseph Owino, Sserkuma wa wili na Murshid.
7. DANNY MRWANDA ABAKI BONGO
Mshambuliaji aliyejiunga na anga baada
ya kucheza michezo saba na Polisi Morogoro Danny Mrwanda, alikuwa
arejea nchini Vietnam lakini aliishia kutua yanga.
Danny Mrwanda baada ya kufanya vyema
katika michezo hiyo 7 ya ligi kuu na kufanikiwa kufunga magoli 4,
alivumishwa kujiunga na Simba SC mara baada ya kuwaaga mashabiki kwa
ajili ya kwenda nchini Vietnam , lakini alirejea nchini na kujiunga
na yanga sc.
Mrwanda alinukuliwa akisema kuwa
alienda Vietnam kwa ajili ya majaribio kabla ya kupata majibu ya
majaribio yake nchini Vietnam alipata ofa kutoka kwa yanga na kuamua
kujiunga nayo.
Inadaiwa kuwa kabla ya kujiunga na
polisi morogoro mwanzoni mwa msimu huu aliomba asajiliwe Simba SC
lakini Simba ikamtolea nnje na kupelekea kujiunga na Polisi Moro.
8. MIKATABA YA WACHEZAJI YASITISHWA.
Imezoeleka dirisho dogo la usajili si
wakati wa kusitisha mikataba lakini safari hii hali imekuwa tofauti
baada ya mikataba 8 ya wachezaji kusitishwa, kata ya hiyo nane upo
mmoja wa mchezaji wa ndani ambaye ni Uhuru Suleiman aliyekuwa
naitumikia Simba SC.
Uhuru Suleiman aliomba mwenyewe mkataba
wake usitishwe na viongozi wa Swimba kuridhia ombi lake na mkataba
wake ukavunjwa bila ya malipo na kuenda kujiunga na Mwadui FC ya
Shinyanga inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
Mchezaji mwingine ambaye inasemekana
aliomba mwenyewe mkataba wake uvunjwe na mshambuliaji wa yanga Jaja
ambaye alii tumikia yanga kwa miezi minne tu na kuomba mkataba wake
uvunjwe na uongozi kuridhia.
Mikataba mingine sita ni vilabu
waliohusika katika uvunjaji wa mikataba ambapo azam FC ilisitisha
mkataba wa Mhaiti Leonel na Mmali Diara, huku yanga waksitisha
mkataba wa Emereson na amisi Kiiza na Simba SC waksitisha mkataba na
Hamsi Tabwe aliyejiunga na yanga na Pierre Kwizera.
Huku kukiwa na taarifa ya Simba SC
kumuondao bila ya kusitisha mkataba, kwenye usajili wao mshambuliaji
aliyemajeruhi Patrick Kiongera ambaye anatarajiwi kurejea uwanjnani
hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment