mtazamo

TFF WAWACHUKULIA HATUA KALI VIONGOZI WALIOHUSIKA KATIKA UDANGANYI FU WA UMRI COPA COCA COLA

Si jambo la kushangaza Afrika kufikisha timu katika hatua ya fainali ya dunia kwa soka la vijana, imekuwa ikifanya hivyo mara kadhaa katika michuano hiyo ya dunia ya vijana na wakati mwingine kutwaa taji la kombe la dunia kwa vijana.

Hali inakuwa tofauti ikifika katika fainali za dunia zisizo husisha mipaka ya umri, mafanikio makubwa ya Afrika katika michuano hiyo ni kufika hatua ya robo fainali, ambapo wametinga mara tatu katika historia ya michuano hiyo kupitia kwa mataifa ya Ghana, Cameroun na Senegal.

Tumepata kushuhudia vizazi vilivyo fanya vizuri katika michuano ya vijana kwa timu za ulaya kuja kufanya vizuri katika timu za wakubwa. Ni nini kinapelekea upande wa Afrika hali iwe tofauti?

Jawabu jepesi wa weza toa kuwa ni udanganyifu wa umri ambao katika soka la Afrika limekuwa jambo la kawaida, kiasi kwamba mtu akikuambia umri wake utamuhoji i umri wa passport ama wa kuwasili duniani.

Ugonjwa huo wa udanganyifu wa umri umepelekea baadhi ya vijana wenye umri unaostahiki kushindwa kushiriki michuano ya copa coca cola iliyomalizika hapo jana kutokana na timu zao za mikoa kuwa na idadi kubwa ya wachezaji waliozidi umri na timu shiriki kuondolewa katika mashindano.
Timu za Mbeya na Mtwara ziliondolewa katika mashindano ya mwaka huu kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji waliozidi umri stahiki ya mashindano na kuwanyima fursa wachache wenye umri unaotakiwa kushindwa kuonyesha huwezo wao na labda wangeweza kupemya katika orodha ya wachezaji watakao uingizwa katika kituo maalum.

Ukiondoa timu hizo zipo timu ziliwabidi wacheze bila ya kuwa na wachezaji wa akiba kutokana na wachezaji wa timu hizo kufutwa katika usahili, miononi mwa timu hizo ni mshindi wa pili timu ya Kinondoni.

Hawa wanao pitisha wachezaji ambao hawana vigezo katika michuano yoyote ile ya vijana ili timu zao ziwe mabingwa ndio wanao haribu malengo ya mashindano husika.

TFF wasiwafumbia macho viongozi wa timu ambao wameleta wachezaji waliozidi umri hata kama ni wameleta mchezaji mmoja ili liwe fundisho wa wengine watakao pewa jukumu la kusimamia timu za mikoa ya vijana kuwa makini na suala la umri wa wachezaji wao kabla ya kufika katika mashindano husika.

Maendeleo ya soka hujengwa na misingi thabiti katika soka la vijana, na hawa wanao chukuwa vijana waliozidi umri katika mashindano ndi wanao tuvurugia program chache za vijana tulizo kuwa nazo nchnini.

Tukisimama kidete kupinga udanganyifu wa umri katika michezo mbalimbali huenda hizi program chache za vijana zikasaidi katika ukuwaji wa soka letu.

Ufundishwaji wa mchezaji aliezidi miaka 17 si sawa na ule aliyokuwa chini ya umri huo, hata katika upande wa tiba pale anapo pata majeraha ni tofauti.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.